Habari za Punde

TANZANIA KUFUNGUA OFISI ZA UBALOZI NCHINI KOREA

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga (kulia) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya dola za Kimarekani 50,000/= sawa na shilingi milioni 108 za Kitanzania zilizotolewa na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum-young leo jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetalewa kwa ajili ya kusaidia kurejesha miundombinu na makazi yaliyoathiriwa na Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 septemba 2016.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msaada wa dola za Kimarekani 50,000/= sawa na shilingi milioni 108 za Kitanzania zilizotolewa na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum-young leo jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetalewa kwa ajili ya kusaidia kurejesha miundombinu na makazi yaliyoathiriwa na Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 septemba 2016.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga (kushoto) akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum-young mara baada ya kupokea msaada wa Dola za Kimarekani 50,000 leo jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetalewa kwa ajili ya kusaidia kurejesha miundombinu na makazi yaliyoathiriwa na Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 septemba 2016. Picha na MAELEZO.
*********************************************************
Na: Frank Shija – MAELEZO.
Tanzania yadhamiria kuimarisha uhusiano baina yake na Jamhuri ya Korea kwa kufungua Ofisi zake za Ubalozi Mjini Seoul, nchini Korea.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga leo jijini Dar es Salaam wakati akipokea msaada wa Dola za Kimarekani 50,000 kwa ajili ya kusaidia urejeshaji wa miundombinu iliyoharibika kutokana na Tetemeko la Ardhi lilitokea Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 Septemba 2016.

Balozi Mahiga amesema kuwa nchi ya Jamhuri ya Korea imekuwa na uhusiano mzuri na wa muda mrefu na Tanzania ambapo kupitia uhusiano huo imekuwa ikisaidia katika mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya akitolea mfano Hospitali za Mloganzila na Chanika ambazo zote zimejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Mahusiano la Korea (KOICA).

“Korea imekuwa na Ofisi za Ubalozi hapa nchini kwa zaidi ya miaka 25 hivyo wameona ni wakati sasa kwa Tanzania kuwa na Ofisi yake Ubalozi nchini nnchini Korea,” Alisema Balozi Mahiga.

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum – Young amesema kuwa msaada huo unatokana na namna ambavyo waliguswa na janga la Tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na makazi ya wananchi.

Ameongeza kuwa msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu na kumpa Pole mnamo tarehe 22 Septemba mwaka huu.

Balozi Song Geum-Young pia amemhakikishia Waziri Mahiga kuwa Korea itaendeleza na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania na kwamba itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa hapa nchini ikiwemo ujenzi wa Daraja la Salender, Meli, Hospitali ya Mloganzila, Chanika na mingineyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.