Habari za Punde

TANZANIA U15 KUKIPIGA NA BURUNDI U15 LEO SAA 1.00 USIKU AZAM COMPLEX

Mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 15 na wale wenzao wa Burundi ambao pia wako chini ya umri wa miaka 15, utafanyika kesho Desemba 18, mwaka huu saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam ulioko, Chamazi, Dar es Salaam.

Muda wa mchezo huo umebadilishwa kutoka saa 10.00 jioni baada ya wadau kadhaa kuomba iwe hivyo ili wapate fursa ya kwenda kushuhudia vijana wa Tanzania ambao watatambulishwa rasmi hiyo kesho mara baada ya kushuhudia michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.

Vijana hao 22 waliokusanywa katika ziara rasmi ya TFF kusaka vipaji mwaka juzi 2014, kwa sasa wanasoma katika Shule za Alliance, Mwanza - kituo ambacho kinawalea kwa ushirikiano kati ya uongozi wa shule hizo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa wiki mbili, walikuwa kambini sehemu mbalimbali kama vile Dar es Salaam, Morogoro na Zanzibar.

Katika ziara hizo, wamepata kucheza mechi za kirafiki tatu ambako Morogoro walicheza mechi moja dhidi ya Moro Kids na kushinda mabao 3-1, kabla ya kwenda Zanzibar na kucheza na Zanzibar Combined ambao mchezo wa kwanza walishinda mabao 10-1 kabla ya mwingine kushinda mabao 16-0. 

Kesho dhidi ya Burundi itakuwaje? ni jambo la kusubiri na kuona lakini Burundi tayari wako jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Azam Tv.

Burundi ilipowasili juzi mchana na ilipokelewa na Kaimu Balozi wa Burundi nchini Tanzania, Bw. Prefere Ndayimshimiye na kuelekea katika Hoteli ya Di Mag iliyopo Mwananyamala Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kirafiki ni maandalizi kwa Tanzania kuijenga Timu Kwaajili ya fainali ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambapo Tanzania itajua mwenyeji wa michuano hiyo ambayo itafanyika mwaka 2019

TFF inatangaza kuwa mchezo huo wa Jumapili hautakuwa na kiingilio ili kuwapa fursa Watanzania kuja kuwashuhudia Vijana wao wakicheza mchezo wao wa kwanza wa Kimataifa.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu wa timu ya vijana weeny umri wa chini ya miaka 14, Oscar Mirambo anayepata ushauri kutoka kwa Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Kim Poulsen kinaundwa na makipa ni Shaban Hassan Kimwaga na Abdulatif Noor Lema.

Walinzi ni Kareem Bakari Mfaume, Asante Hamis Bwatam, Rashid Hamisi Rashid, Moris Michael Njako, Harubu Juma Tanu, Cosmas Lucas Jakomanya, Salim Abubakar Lupepo na Dastan Daniel Matheo.

Viungo ni Edson Jeremiah Mshirakandi, Jonathan Raphael Kombo, Alphonce Mabula Msanga, Erick Boniface Bunyaga, Gssper Godfrey Gombanila, Sabri Dahari Kondo na washambuliaji ni Jafari Juma Rashid, Ludaki Juma Chasambi, Steven Emmanuel Sodike, Michael Mussa Mpubusa na Edmund Geofray John.

Timu hii inaundwa na vijana ambao TFF iliwakusanya tangu 2014 na kuwaunganisha kwa pamoja katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Kukuza Vipaji ya Alliance iliyoko Mwanza. Mbali ya kutoa elimu ya msingi na sekondari, pia Alliance inatoa elimu ya awali kwa watoto wa kuanzia umri wa miaka miwili hadi sita.

Timu hii inaandaliwa kuja kwa time mpya ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ambao watashiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana mwaka 2019 ambako Tanzania imeteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa mwenyeji. Kambi itavunjwa Desemba 19, mwaka huu.

Kikosi cha Burundi kinaundwa na Harerimana Jean Marie, Habuka Papy, Habonimana Eric, Masumbuko Jules, Hakizimana Ulimwengu, Mossi Djuma, Nkeshimana Nuru, Hakizimana Assumani, Habonimana Pacifique.

Wengine ni Irankunda Arsene, Munaba Edson, Bukuru Samir, Mugisha Axcel, Kirimwovyinshi Abdillah, Niyonkuru Cedric, Manirankunda Styve Mugisha Richard na Mugisha Simplice.

Viongozi waliokuja na timu ni Rwabayinkovu Emile, Nahimana Issa, Buduri Jeannette, Kanega Alphonse, Jumapili Hassan, Rubanganya Jean Paul, Riziki Jacob.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.