Habari za Punde

TIMU YA MBAO FC YAINGIA MKATABA WA UDHAMINI NA KAMPUNI YA HAWAII KUPITIA COWBELL

 Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Hawaii Products Suplies Ltd, Said Ali Khamis (kushoto) akimkabidhi sehemu ya jezi, Mwenyekiti wa Timu ya Mbao Fc, Solly Njash, wakati wa hafla ya kutiliana saini Mkataba wa udhamini kati ya kampuni hiyo na timu hiyo wenye thamani ya Sh. M. 25. Hafla hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo kwenye Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF. Kampuni hiyo imeidhamini timu ya Mbao Fc kupitia Bidhaa ya Maziwa Bora ya Cowbell.
 Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Hawaii Products Suplies Ltd, Said Ali Khamis (kushoto) akimkabidhi sehemu ya jezi, Mwenyekiti wa Timu ya Mbao Fc, Solly Njash, wakati wa hafla ya kutiliana saini Mkataba wa udhamini kati ya kampuni hiyo na timu hiyo wenye thamani ya Sh. M. 25. Hafla hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo kwenye Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF. Kampuni hiyo imeidhamini timu ya Mbao Fc kupitia Bidhaa ya Maziwa Bora ya Cowbell.
 Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Hawaii Products Suplies Ltd, Said Ali Khamis (kushoto) akisainiana mkataba wa udhamini na Mwenyekiti wa timu ya Mbao Fc, Solly Njash, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ofisi za TFF leo mchana.
 Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Hawaii Products Suplies Ltd, Said Ali Khamis (kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini na Mwenyekiti wa timu ya Mbao Fc, Solly Njash, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ofisi za TFF leo mchana.
 Mwenyekiti wa timu ya Mbao Fc, Solly Njash,akizungumza na waandishi wa habari.
TIMU ya Mbao Fc ya jijini Mwanza leo imeingia mkataba wenye thamani ya Sh. Milioni 25 na Kampuni ya Hawaii Products Suplies Ltd, kupitia Maziwa Bora ya Cowbell.
Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo ya kutiliana saini mkataba wa udhamini, Mhasibu Mkuu wa Kampuni hiyo, Said Ali, alisema kuwa udhamini huo unaweza kuongezeka kulingana na jinsi timu itakavyokuwa ikifanya vizuri katika mashindano ya Ligi Kuu Bara.

Timu hiyo ya Mbao Fc, i
liyopanda daraja msimu huu, imeweza kuhimili mikiki ya Ligi Kuu katika mzunguko wa kwanza na kufanya vizuri katika msimamo wa Ligi na 
kuwa na matokeo chanya.

Akizungumza wakati wa utiaji saini, Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njashi amesema kuwa mkataba huo utawasaidia hasa katika maandalizi ya timu yao na zaidi kiwango cha fedha kinaweza kuongezeka kutokana na matokeo watakayokuwa wanayapata kwenye ligi.

Njashi amesema kuwa, hatua hiyo ni moja ya hatua kubwa kwa timu yao kutokana na hali halisi ya kifedha inayozikabili timu changa.

''Kwa ku
pata udhamini huu hivi sasa tunategemea kufanya vizuri kutokana na morari na kuwapa moyo wadhamini wetu chini ya Kocha wetu, 
 Etien Ndailagije mwenye malengo ya kuinua zaidi vipaji vya Vijana''. alisema Njash

Kwa upande wa Meneja Masoko Hawaii, Erisalia Ndeta amesema kuwa wameridhishwa na kiwango cha Mbao Fc mpaka kufikia hatua ya kuwapatia udhamini huo wa miezi sita ila wanatarajia utakuwa ni endelevu kwani wana imani wataendelea kufanya vizuri.

Ndate amesema kuwa, udhamini huo unaweza kuongezeka zaidi kulingana na kiwango cha timu kitakavyokuwa kwani huu ni mwanzo tu na wanaweza kufanya mengi zaidi.

Mbao imefanikiwa kupata udhamini huo baada ya kuweza kuonyesha kandanda safi zaidi, kwa sasa timu hiyo ipo kambini na inatarajiwa kuondoka Jumapili asubuhi kuelekea Rorya kucheza na Stone Sugar ya nchini Kenya ikiwa ni moja ya maandalizi.

WAKATI HUO HUO: Timu hiyo ya Mbao Fc, imeanza rasmi kambi kwa ajili ya 
 kujiandaa na ligi kuu Bara raundi ya 
pili kwa kuvaana na Stone Sugar ya nchini Kenya, katika mchezo wa kirafiki.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.