Habari za Punde

UKOSEFU WA HUDUMA YA KWANZA VIWANJA VYA MIKOANI NI TATZO KUBWA

Zainab Nyamka, Dar
BAADA ya kufariki uwanjani kwa mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao FC Ismail Khalfan siku ya Jumapili ya December 4, Hospitali wametoa ripoti ya kilichosababisha kifo cha mchezaji huyo wakati wa mchezo kati ya Mbao FC dhidi ya Mwadui FC.

Ripoti iliyotolewa na hospitali ya mkoa wa Kagera kuhusiana na kifo cha mchezaji huyo, kupitia kwa jeshi la Polisi, Ismail alifariki uwanjani kutokana na kupata tatizo la kusimama ghafla kwa moyo (Sudden Cardiac Arrest-SCA).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Augustin Ollomi ametoa taarifa baada ya uchunguzi wa madaktari kuhusu kifo cha mchezaji huyo ambaye hakuwa na jeraha lolote ila baada ya uchunguzi walibaini kusimama ghafla kwa moyo (Sudden Cardiac Arrest) kulisababisha kifo.

Kulifunguliwa jalada la uchunguzi, bahati nzuri madaktari walifanya huduma ya haraka, kwa mwonekano huyu marehemu Ismail Mrisho Khalfan ambaye ndiye alikuwa ameanguka pale uwanjani kwa nje hakuonekana kuwa na jeraha kwa hiyo madaktari wakatueleza lazima afanyiwe uchunguzi wa kina.

Kutokana na tatizo hilo, Ismail alitakiwa kupatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuanguka kwa kupata msaada ni kupata electrical shock ili kushtua mfumo wa umeme wa moyo, na hii inapaswa kufanyika ndani ya sekunde chache baada ya kubainika kuanguka na ukisimama bila kurudi katika hali yake unasababisha kifo ndani ya sekunde chache.

Kitaalamu kawaida moyo una mfumo wa umeme (heart electrical system), ambao unadhibiti mapigo ya moyo, mfumo huu ukisimama basi moyo unashindwa kusukuma damu sehemu muhimu kama ubongo na ogani kuu.

Ukosefu wa vifaa uwanjani ikiwemo daktari mkuu wa uwanja na gari la wagonjwa limekuwa kama wimbo wa taifa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kwa kushindwa kuwa na vifaa hivyo na pale mchezaji anapotokea anapata tatizo anashindwa kupata huduma kwa usahihi na wakati muafaka ,na ikumbukwe katika msimu huu wa ligi kuu Vodacom, Golikipa wa timu ya African Lyon aliweza kuvunjika mbavu katika mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu lakini hakukuwa na gari ya wagonjwa na aliishia kubebwa kwenye gari aina ya Pick up.

Tumeshuhudia mchezaji wa Stand United Chidiebele akiumia uwanjani na kuvunjika taya lakini hakukuw ana huduma ya uhakika achilia hao wapo wachezaji wengi wanaopata madhara ila uhakika wa huduma katika viwanja vya mikoani ni mdogo sana na hata katika ripoti za waamuzi wamekuwa wakiandika kutokuwepo kwa gari la wagonjwa ila hakuna jitihada zinazofanywa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.