Habari za Punde

UTAMADUNI CHANYA WA KUFIKIRI NI NTA YA MAENDELEO KWA VIJANA.

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala akiongea na wahitimu (hawapo pichani) wa Programu ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) unaoendeshwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya TechnoServe wakati wa Mahafali ya pili ya vijana waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua kuhusu jitihada za Serikali katika kuwawezesha vijana wakati wa Mahafali ya pili ya vijana waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali mkoani Mbeya. Mafunzo hayo yapo chini ya Programu ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) unaoendeshwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya TechnoServe. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

Meneja wa Programu ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) Catherin Musangi akitoa taarifa ya mradi huo kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala wakati wa Mahafali ya pili ya vijana waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali mkoani Mbeya.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akimpongeza mhitimu wa mafunzo ya Programu ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) Irene Mwasile (mwenye mlemavu) mwenye umri wa miaka 27 kutoka kikundi cha Umasikini Kwaheri Shilanga, kata ya Ilembo mkoani Mbeya.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akimpongeza mhitimu wa mafunzo ya Programu ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) Irene Mwasile (mwenye mlemavu) mwenye umri wa miaka 27 kutoka kikundi cha Umasikini Kwaheri Shilanga, kata ya Ilembo mkoani Mbeya.
 Baadhi ya wahitimu wa Programu ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) akimsikiliza Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala wakati wa Mahafali ya pili ya vijana waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali mkoani Mbeya.
 Baadhi ya wahitimu wa Programu ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) akimsikiliza Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala wakati wa Mahafali ya pili ya vijana waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali mkoani Mbeya.
 Baadhi ya wahitimu wa Programu ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) akimsikiliza Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala wakati wa Mahafali ya pili ya vijana waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali mkoani Mbeya.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala (katikati aliyevaa tai) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Programu ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE). Kushoto Mkuu wa Mkoa ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel. Picha na Eleuteri Mangi-WHUSM, Mbeya
***************************************************
Na Eleuteri Mangi-WHUSM, Mbeya
Vijana wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia, kuboresha na kuimarisha utamaduni wa namna ya kufikiri kwa mtazamo chanya ili waweze kujitambua na kutumia fursa walizonazo katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala wakati wa Mahafali ya pili ya vijana waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali kupitia Programu ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) unaoendeshwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya TechnoServe.
Katika mahafali hayo, vijana 907 kutoka Mbeya jiji na Mbeya vijijini wamehitimu na kunufaika na mafunzo ambayo yamewawezesha kubadili utamaduni wa namna ya kufikiri hatua ambayo ni mkombozi wa maisha yao katika kujiletea maendeleo endelevu.
“Ni vema kuwaza kwa mtazamo chanya badala ya mtazamo hasi, huu ni muda wenu muafaka wa kubadili maisha yenu baada ya kuhitimu mafunzo haya, ni lazima kubadilika” alisema Makala.
Mkuu huyo wa mkoa awasisitiza vijana hao kutumia elimu waliyoipata ya namna ya kuweka akiba ili waweze kufanya biashara zenye tija katika maisha yao pamoja na kuwahimiza watumie fursa zilizopo katika maeneo yao kwa kubadili changamoto zinazokabili jamii wanamoishi kuwa fursa ambazo kwa ndio njia ya kunyanyua vipato vyao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewapongeza Taasisi ya TechnoServe kwa kuwa mstari wa mbele kwa kushughulika na vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa kwa kubadili utamaduni na fikra zao katika kuwekeza kwenye wajasiriamali wenye tija katika maisha yao.
Prof. Ole Gabriel ameongeza kuwa Taasisi ya TechnoServe imekuwa mkombozi kwa vijana wote bila kujali tofauti zao za kijinsia, hali walizonazo kiuchumi pamoja na vijana wenye mahitaji maalum kwa kuzingatia kila mtu anauwezo ndani yake akielimishwa ni rasilimali kubwa ya taifa katika kupambana na umasikini wa fikra na kipato.
Aidha, Prof. Ole Gabriel amempongeza kijana Irene Mwasile (mwenye ulemavu) kutoka kikundi cha Umasikini Kwaheri Shilanga, kata ya Ilembo mkoani Mbeya kwa kuwa miongoni mwa vijana waliofanya vizuri katika mafunzo hayo kwa kuandika andiko mradi  bora na kuwa miongoni mwa kundi la vijana walioshika nafasi ya kwanza na kuzawadiwa mtaji wa shilingi 550,000 pamoja na cheti.
Kwa upande wake mshindi huyo amesema kuwa anaishukuru Taasisi ya TechnoServe kwa kumpa mwanga katika maisha yake, hadi sasa ameanzisha mradi wa kufuga kuku ambao idadi yake hadi sasa ni 30 na matarajio yake ni kuwa mfugaji wa bora wa kuku nchini na hata barani Afrika.
Katika mahafali hayo vijana wengine waloshinda katika nafasi tatu za juu wanatoka katika vikundi 30, vikundi 16 vipo Mbeya jiji na vikundi 14 vipo Mbeya Vijijini, washindi katika vikundi hivyo wamegawanyika katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza washindi wamezawadiwa mtaji wa shilingi 550,000, washindi wa pili shilingi 350,000 na washindi wa tatu shilingi 200,000
Hadi sasa mradi wa STRYDE mkoani Mbeya umewafikia vijana 2193 katika kuwajengea uwezo kiuchumi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2014 ambapo TechnoServe inatarajia kuwafikia vijana 15,430 ifikapo 2019.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.