Habari za Punde

(VIDEOLINK) MANISPAA YA KIGOMA UJIJI KUTEKELEZA KWA VITENDO MPANGO WA UENDESHAJI KWA UWAZI (OGP)


Na Jonas Kamaleki, Paris.
Manispaa ya Uijiji Kigoma imeazimia kuwashirikisha wananchi wake katika mipango ya maendeleo na kubadli utamaduni uliokuwepo wa kuitegemea Serikali kuwaletea mipango yake.

Hayo yamesemwa jana Jijini Paris  na Mratibu wa Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) Kigoma, Mhandisi Sultan Ndaliwo wakati wa kufunga Mkutano wa Kilele wa mpango huo OGP.

Mhandisi Ndaliwo amesema ushirikishwaji huo utasaidia kutatua changamoto zinazojitokeza kwa wananchi bila kuwepo kwa ukiritimba kwani masuala hayo yatakuwa yanajulikana wazi kwa wananchi.

"Nimefurahishwa na jinsi jiji la Paris linavyowashirikisha wananchi wake katika kupata maendeleo yao jambo ambalo tutaenda kulitumia Kigoma," alisema Ndaliwo.

Ameongeza kuwa anaamini Kigoma Ujiji inakwenda kubadilika kutokana na utekelezaji wa Mpango Mkakati waliojiwekea unatekelzwa ipasavyo.

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Ujiji Kigoma, Sultani Hussein Luhavi amesema ataenda kuweka mfumo wa utoaji taarifa kwa haraka ambapo kunatokea tatizo katika eneo lolote ndani ya Manispaa ili lifanyiwe kazi na wahusika (tracking system).

Amezishauri Manispaa nyingine zijenge utamaduni wa kuwasilkiliza wananchi na kuwashirikisha ipasavyo katika mipango ya maendeleo.

"Utendaji wa jinsi hii utabadilisha Manispaa yetu na kuifanya ipige hatua kubwa katika maendeleo," alisema Luhavi.

Luhavi amezitaka Manispaa na Halmashauri za Miji nchini kuiga mfano wa Manispaa ya Ujiji Kigoma ili kuharakisha maendeleo yao.

Halmashauri ya Manispaa ya Ujiji Kigoma ni Kati ya Manispaa 15 duniani zilizojiunga na OGP kama manispaa na si nchi.

Manispaa nyingine zilizojiunga na Mpango huo ni pamoja na  Austin ya Marekani; Bojonegoro, Indonesia; Buenos Aires, Argentina; Elgeyo Marakwet, Kenya; Jalisco, Mexico; La Libertad, Peru; Madrid, Spain; Ontario, Canada;

 Paris, France; Sao Paulo, Brazili; Scotland, Uingereza; Sekondi-Takoradi, Ghana; Seoul, Korea Kusini and Tbilisi, Georgia.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.