Habari za Punde

VIJANA WA SIMBA U-20 WATWAA UBINGWA LIGI YA VIJANA

TIMU ya vijana ya Simba ya U-20, imeibuka kidedea katika mashindano ya timu za vijana wa U-20yaliyomalizika jana kwenye Uwanja wa Chamaz jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na Mtandao huu,Kocha mkuu wa timu hiyo baada ya kumalizika mchezo huodhidiya Azam Fc, Kiondo alikiri kuwa mchezo huohaukuwa rahisi kwake kutokana na wapinzani pia kuwa wazuri.

Simba waliibuka kidedea baada ya kuwagalagaza wapinzani wao kwa mikwaju ya penati 5-3 baada ya kumalizika dakika 120 kwa sare ya mabao 2-2.

“Namshukuru Mungu pia wachezaji wangu kwani walijituma na kuhakikisha wanachukua ubingwa, wanastahili pongezi kwa sababu walijitoa na kupigana kufa na kupona,” alisema Kiondo

Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), timu zote zilionyesha kandanda safi na lililojaa ufundi.

Simba walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 14 lililofungwa na Moses Kitandu akimalizia pasi ya George Emmanuel, lakini Shaaban Iddi akaisawazishia Azam FC dakika ya 28.

Dakika ya 57, Said Mohammed akaifungia Azam FC bao lakini Said Hamisi isawazishia Simba dakika ya 83 na kumalizika dakika 90 kwa sare 2-2 hivyo zikaongezwa dakika 30 zilizomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Penalti za Simba zilifungwa na Calvin Faru, Said Hamisi, Mokiwa Perus, Vincent Costa na Moses Kitandu, wakati za Azam zilifungwa na Abbas Kapombe, Rajab Mohammed na Adolph Bitegeko huku ya Said Mohamed ikipanguliwa na kipa wa Simba, Ally Salum.

Katika mchezo wa nusu fainali, Simba iliitoa Stand United kwa penalti 8-7 baada ya sare ya 1-1 wakati Azam iliitoa Mtibwa Sugar kwa penalti, 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120.

Hii ni ligi ya kwanza ya vijana kuchezwa hapa hapa nchini ikishirikisha timu 16 zilizoanzia kwenye hatua ya makundi katika Kituo cha Kagera na Dar es Salaam.

Ligi hiyo imemalizika huku ikiacha kumbukumbu ya kuhuzunisha kufuatia kifo cha mchezaji wa Mbao FC, Ismail Mrisho Khalfan, aliyefariki wakati timu yake ikicheza na Mwadui FC baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui.

Ismail (19) alifariki Desemba 4, Bukoba baada ya kuanguka uwanjani dakika ya 74 Uwanja wa Kaitaba, dakika chache baada ya kuifungia bao timu yake katika ushindi wa 2-0 na akazikwa nyumbani kwao Mwanza siku iliyofuata.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.