Habari za Punde

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAZINDUA HUDUMA YA ULIPAJI WA MAFAO YA FIDIA NA UZINDUZI WA UBIA BAINA YA WCF NA WATOA HUDUMA ZA AFYA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akikata utepe kuzindua mafao ya Fidia na ubia baina ya watoa huduma za afya .Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mhagama kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam, Desemba 20, 2016. wanaoshuhudia ni Naibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mh. Anthony Mavunde, (wapili kulia), Mh. Dkt. Abdallah Possi, (watatu kulia), Bw. Emmanuel Humba, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wanne kulia, na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba. (watano kulia). .( PICHA NA MUHIDIN SUFIANI)
Na Ripota wa Sufianimafoto Blog, Dar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge kazi ,vijana Ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Muhagama, amewataka waajili wote kuwasilisha Michango ya wafanyakazi wao Mfuko Fidia kwa Wafanyakazi WCF kwa wakati.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Huduma za utoaji wa Mafao ya fidia kwa wafanyakazi na ubia kati ya Mfuko na watoa Huduma za Afya amesema kuwa
kwa Mwaka huu wafedha Serikali imewasilisha Michango ya wafanyakazi wake wote ambapo alizitaka Sekta binafsi pia kuwasilisha Michango yao kwa wakati.

Sanjari na Hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Masha Mshomba ameongeza kuwa Mpaka kufikia Novemba 30 Mwaka huu Jumla ya waajili 5945 wamechangia na wamepewa na ya usajili.

Hata Hivyo Mweketi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko huo Emmanuel Humba amesema Mfuko Huo utachangia kwa kiwango kikubwa Sera ya Tanzania ya Viwanda iliyoa anzishwa na Serikali ya awamu ya tano kwani wafanyakazi watakapo kuwa na Afya njema watafanya kazi kwakujiamini na kuleta Maendeleo.
Waziri Mhagama akihutubia
Mwenyekiti wa bodi ya WCF, Bw. Emmanuel Humba akitoa hotuba yake
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba, akitoa hotuba yake
Mgeni rasmi, Naibu Mawaziri, viongozi wa WCF, na waliotunukiwa vyeti wakiwa kwenye picha ya pamoja

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Jenista Mhagama, akimkabidhi Cheti cha utoaji huduma bora za afya,  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bernard Konga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Jenista Mhagama, akimpongeza msanii wa muziki wa kizazi kipya,Mrisho Mpoto kwa kufanya kazi nzuri ya ubalozi na kuutangaza Mfuko huo. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAZINDUA HUDUMA YA UTOAJI MAFAO YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KATI YA MFUKO NA WATOA HUDUMA ZA AFYA.

Picha ya pamoja na wasanii wa bendi ya Mjomba 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Jenista Mhagama, akimkabidhi Cheti cha utoaji huduma bora za afya,  Mkuu wa Idara ya Utawala wa Hospitali ya Muhimbili, Leilla William, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.
 Picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko huo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Jenista Mhagama, akimkabidhi Cheti cha utoaji huduma bora za afya,  Mkurugenzi Mtendaji wa ‘Muhimbili Orthopaedic Institute’ Dkt. Othman Kiloloma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.
 Picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko huo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Jenista Mhagama, akimkabidhi Cheti cha utoaji huduma bora za afya,  Mwakilishi wa Stratage Insurance, Dkt. Aisha Ahmed, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.
 picha ya pamoja
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Jenista Mhagama, akimkabidhi Cheti cha utoaji huduma bora za afya,  Mwakilishi wa AAR, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.
 Picha ya pamoja na wakurugenzi wa Mifuko ya kijamii
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Jenista Mhagama, akimkabidhi Cheti cha utoaji huduma bora za afya,  Mkuu wa Kitengo cha Tiba wa Jubilee Insurance, Keneth Agunda,  wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa WCF, Mosha Mshomba, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Mgeni rasmi akisalimiana na baadhi ya viongozi
 Baadhi ya wafanyakazi wakijipanga kumpokea mgeni rasmi
 Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Jenista Mhagama, akizungumza jambo na Mbunge wa Dodoma, Anthony Mavunde.

 Wasanii wa Kikundi cha Mjomba Band wakiigiza 
 Maigizo yakiendelea
 Sehemu ya washiriki na wadau katika uzinduzi huo.
 Maigizo yakiendelea
 Mrisho Mpoto akiimba wimbo maalum wa kuelimisha juu ya Mfuko huo.
 Badhi ya wafanyakazi wa Mfuko huo wakipongeza yaliyokuwa yakiendelea ukumbini hapo
 Mwimbaji Banana Zorro akiimba
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka, akiwa ukumbini humo
 Wafanyakazi wa WCF wakipongeza jambo

 Anthony Mavunde akizungumza
Baadhi ya warembo waliokuwa wakitoa huduma katika hafla hiyo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.