Habari za Punde

WADAU WA KILIMO WAKUTANA KATIKA KONGAMANO LA KILIMO MJINI DODOMA

Na: Tulinkisa Ndelwa na Hawa Mohamed, Dodoma
Mwanzoni mwa mwezi Desemba 2016 lilifanyika Kongamano kubwa la Mwisho wa 
Mwaka lililowahusisha Wadau Wa Kilimo, uvuvi na Viwanda wakiwemo wawakilishi 
wa wakulima, Mashirika binafsi, Wanahabari na Maafisa kutoka Wizara 
mbalimbali,

Lengo kuu ni kuangazia uwezeshaji wa Viwanda katika sekta ya kilimo na
namna ambavyo kilimo kinaweza kuchagiza katika ongezeko la viwanda katika
kufikia mafanikio ya Kuwa na serikali yenye uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 
2025 . 

Mkurugenzi wa ANSAF (Agricultural Non state Actors Forum), Audax
Rukonge alisema kwa mwaka 2017, miongoni mwa mambo watakayo yazingatia ni 
pamoja mifumo ya kilimo, kuinua maisha ya watanzania, na mabadiliko ya
mitazamo ya wadau.

Katika hatua nyingine Rukonge alisema ili nchi iwe ya viwanda ni lazima
kuongeza tija katika sekta mama ambayo ni kilimo.Tanzania imekuwa
ikitegemea mvua katika kilimo sambamba na tekinolojia duni pamoja na
kutegemea wakulima wadogo. Takwimu ya tija ambayo inapatikana kutoka
mashambani ipo chini ya nusu.hivyo ni vigumu kufikia lengo la Tanzania ya
uchumi wa kati yaani Tanzania ya viwanda kama sekta mama haitainuliwa.
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dr Charles Tizeba,ambaye alimuwakilisha
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kongamano hilo, Alisema anasikitishwa na 
mikakati mingi ambayo imekuwa ikitolewa kila mwaka na kutokufanyiwa kazi. 

Na kwamba azma ya serikali haiwezi kufikiwa ikiwa mikakati haifanyiwa kazi.
“Ni kweli kwamba katika kufikia lengo la viwanda lazima kuangalia malighafi
itatoka wapi”. Alisema Tzeba.

Katika utafiti uliofanyika mwaka 2013 ulionyesha kwamba Tanzania ilipoteza
kiwango cha fedha ya kimarekani dola 550 kwa kupeleka malighafi nje
(korosho), kwa kuwa na teknolojia duni ya uchakataji. Na katika mwaka
2014/15, Tanzania iliagiza mafuta yenye thamani ya fedha ya kimarekani dola
mil. 357. 

Ikiwa mikoa ya Singida, Iringa, na Mbeya inauwezo wa kuzalisha
kiwango kikubwa cha alizeti kuliko ambavyo mikoa hiyo imekuwa ikizalisha.

Hali ambayo inapelekea kuagiza kiwango kikubwa cha mafuta kutoka nje.
Pia 
Tanzania imekuwa ni nchi ya pili chini ya jangwa la sahara kuwa ni nchi
yenye wingi wa mifugo,lakini imekuwa ikitegemea maziwa na ngozi kutoka nje.

Asilimia kubwa ya wananchi wanashughulika na kilimo, lazima iwekwe mikakati 
madhubuti ambayo itahakikisha ongezeko la uzalishaji wenye tija, ilikufikia 
lengo la viwanda.

“Naamini vijana wakiingia kwenye kilimo kwa kuamua wenyewe. Na siyo
kwasababu ya kukosa ajira.Vijana wakitoka vyuoni na mitaani wakaamua
kuingia kwenye kilimo tutafika mbali sana. Niko tayari kupambana na
changamoto zilizopo ili kuwafanya vijana wafurahie sekta ya kilimo.

Vijana 
walio tayari kuingia kwenye kilimo wajiunge kwenye vikundi ,naahidi kuwapa 
mashamba na kuwatafutia fursa za mikopo.”Alisema waziri Tzeba
Kwa hali hii, ili kufikia lengo la viwanda ni lazima kuinua uzalishaji wa
ndani na kuongexza tija kwenye srkta mama ambayo ni kilimo, Usafirishaji,
elimu bora,mazingira rafiki ya uwekezaji na mfumo mzuri wa uwekezaji kwa
kuwa wawekezaji wengi wanaangalia wenye utayari katika mfumo wa kuwekeza.

Ni vyema serikali ikaendeleza nia na madhumini ya sera ya *KILIMO KWANZA*.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.