Habari za Punde

WAKAGUZI WA NDANI WATAKIWA KUSIMAMIA UBORA WA MIRADI MIKUBWA YA UJENZI WA MIUNDOMBINU

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (kulia), akimsikiliza   Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi (kushoto) wakati akielezea mafanikio na changamoto zinazokikabili chuo hicho.  Kushoto kwa Mkuu wa Chuo ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw.  Mohamed Mtonga, Msaidizi wa Mkuu wa Chuo Dkt. Samwel Werema, Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi– Ukaguzi Mamlaka za Mitaa Bw. Mwanyika Musa na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Kiufundi Bw. Amin Mcharo
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi aliyesimama akitoa utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo kwa wakaguzi wa Ndani kutoka Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed Mtonga, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Kiufundi Bw. Amin Mcharo na kulia kwa Kaimu Mkuu wa Chuo ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali – Ukaguzi mamlaka za mitaa Bw. Mwanyika Musa. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

 Wakaguzi wa Ndani kutoka Serikali za Mtaa na Sekretarieti za Mikoa wakiwa kwenye mafunzo ya ukaguzi, Mgeni Rasmi katika mafunzo hayo ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika. Mafunzo haya yanafanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, mkoani Arusha.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (aliyesimama) akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa ndani ambapo alisema mpaka sasa wakaguzi wa ndani 308 wamepata mafunzo hayo na wakaguzi 32 wameshafanya mafunzo hayo kwa vitendo.
 Wakaguzi wa Ndani kutoka Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa katika picha ya pamoja. Waliokaa ni Mgeni Rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Kiufundi Bw. Amin Mcharo na kushoto kwake ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed Mtonga na Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali – Ukaguzi mamlaka za mitaa Bw. Mwanyika Musa.
 Mgeni Rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (katikati) wakibadilishana mawazo na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi (Kushoto) na kulia ni  Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed Mtonga.
**********************************************************
Benny Mwaipaja, WFM, Arusha
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika, amewataka wakaguzi wa ndani nchini kuhakikisha kuwa miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara na majengo yanajengwa kwa ubora unaolingana na thamani ya rasilimali fedha iliyotumika.

Bi. Mwanyika ametoa rai hiyo Jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya wakaguzi wa ndani kutoka Halmashauri za wilaya na Sekretarieti za mikoa iliyoko Kanda ya Kaskazini, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara
Amesema kuwa wabunge na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakilalamikia miradi mingi mikubwa ikijengwa chini ya kiwango na kuisababishia serikali hasara kubwa kutokana na usimamizi mbovu unaofanywa na mamlaka na idara za serikali wakiwemo wakaguzi wa ndani.

“Nina Imani kuwa mafunzo mnayoyapata ya namna ya kukagua ubora wa miradi mikubwa inayotumia fedha nyingi za serikali yatasaidia kuokoa fedha na kuifanya miradi inayojengwa idumu muda mrefu” aliongeza Bi. Mwanyika.

Kwa upande wake Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali Bw. Mohammed Mtonga, amesema kuwa kuanzishwa kwa mafunzo hayo yanayofadhiliwa kupitia mradi wa kuboresha Mifumo ya Fedha (PFMRP), yanatokana na mahitaji makubwa ya ujuzi wa namna ya wakaguzi wa ndani wanavyoweza kutambua ubora wa miradi mikubwa ya ujenzi inayotekelezwa hapa nchini kama inakidhi viwango.

“Wakaguzi hawa si wataalamu wa masuala ya ukandarasi lakini uwezo wanaojengewa ni pamoja na kupelekwa kwenye miradi mikubwa ya uejnzi ikiwemo barabaraba ambapo wataelekezwa namna ya kutambua miradi ambayo haikidhi viwango na kutoa ushauri kwa watoa maamuzi ili kuokoa fedha ya serikali isipotee” aliongeza Mtonga.


Wakaguzi wa ndani 302 kutoka Halmashauri na Sekretarieti za Mikoa nchini wamepatiwa mafunzo hayo ambapo pamoja na mafunzo ya nadharia, wakaguzi hao wa ndani wamefundishwa kivitendo namna ya kutambua miradi iliyojengwa chini ya viwango

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.