Habari za Punde

WANANCHI WA SINGIDA KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME WA UPEPO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa umeme kujadili mkakati ya kuzalisha nishati ya Umeme kwa njia ya Upepo leo katika ukumbi wa Hotel ya Hyatt Jijini Dar.
***************************************************
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mh. January Makamba amesema kuwa mpango wa serikali ni kuwa na vyanzo vingi vya uzalishaji umeme ili kuwa na vyanzo vya nchi endelevu na kuunga mkono juhudi za benki ya dunia kuzalisha umeme wa upepo katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Makamba amesema hayo wakati wa Kongamano la wadau wa Nishati ya umeme walipokutana kuzungumzia matumizi ya Nishati ya umeme inayozalishwa kwa njia ya upepo itakayounganishwa kwenye gridi ya taifa na mfumo huo utawasaidia wananchi wa Singida .

"Kwa kuwa umeme huo utazalishwa kwenye maeneo ya vijijini, wananchi wanatakiwa kupata umeme kwa bei rahisi kulingana na uchumi wao na sio kuuziwa umeme kwa bei juu, na zaidi Wizara yake inapenda kuweka wazi kuwa huu mradi una faida kubwa sana kulingana na mfumo wa nchi ulivyo,"amesema Makamba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha umeme wa upepo Afrika Mashariki Six Telecoms, Rashid Shamte amessema kuwa mfumo huu wa gridi ndogondogo una faida kubwa sana kwa wananchi kwani asilimia kubwa kulingana na ripoti ya benki ya dunia wananunua umeme wa bei nafuu kwahiyo serikali imekubaliana na kampuni yetu na imeweza kukubali kuwa mradi huu una tija na utasimamiwa na serikali yenyewe kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida pamoja na Halmashauri.

Shamte ameendelea na kusema, kwa Phase ya kwanza watatoa umeme megawati 100 na itaendelea mpaka kufika megawati 300 na wataunganisha kwenye gridi ya taifa, na huu mradi utakuwa na faida kwa wananchi pamoja na wale watakaotolewa kwenye maeneo yao watafaidika kwa kulipa stahiki zao.

Kwa upande wa Wizara ya Nishati na Madini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo amewataka wawekezaji hao kuuza umeme kwa bei rahisi kwani mara nyingi mipango ya serikali imekuwa haiendani na mikakati ya wawekezaji kwahiyo wanategemea kuona kuwa mradi huu uwe nafuu ya wananchi wa vijijini kupata umeme kwa bei rahisi.
Mkurugenzi Mtendaji Six Telecoms, Rashid Shamte (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye kongamano la wadau wa umeme wenye lengo la kuzalisha umeme wa nguvu ya Upepo wenye lengo la kuanza kuzalisha umeme katika mkoa wa Singida.
Baadhi ya wadau wakiwa kwenye kongamno la wadau wa umeme 
Mkurugenzi Mtendaji Six Telecoms, Rashid Shamte akizungumzia uzalishaji wa umeme kwa njia ya upepo utakaosimamiwa na Kampuni ya kuzalisha umeme huo ya Afrika Masharikana awamu ya kwanza itaanzia mkoani Singida. 
Alex Moulds kutoka Energy Net Limited akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuzalisha umeme wa Upepo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.