Habari za Punde

​WAOGELEAJI WA DAR SWIM CLUB WATAMBA KWENYE MASHINDANO YA VIJANA

 Waogeleaji chipukizi wakishindana katika mashindano ya vijana
Muogeleaji chipukizi akishindana katika mashindano ya vijana. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

 Waogeleaji wakipozi baada ya kushinda medali katika mashindano ya vijana
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye  akizungumza na mmoja wa viongzoi wa Chama Cha Kuogelea nchini (TSA), Imani Dominic kabla ya kuwazawadia waogeleaji wa Dar Swim Club,  Marin de Villard, Emmanuel Moroni, Maia Tumiotto na Chichi Zengeni baada ya kushinda katika mashindano ya vijana ya Dar Junior.
 Waogeleaji wakipozi baada ya kushinda medali katika mashindano ya vijana
 Muogeleaji chipukizi akishindana katika mashindano ya vijana
  Waogeleaji wakipozi baada ya kushinda medali katika mashindano ya vijana
 Waogeleaji wakipozi baada ya kushinda medali katika mashindano ya vijana
Waogeleaji wakipozi baada ya kushinda medali katika mashindano ya vijana
*********************************************
Na Mwandishi wetu, Dar
Klabu ya kuogelea ya Dar Swim Club (DSC) imeibua katika nafasi ya kwanza kwa upande wa waogeleaji mmoja mmoja ya umri chini ya miaka 13 yaliyomalizika hivi karibuni.
Klabu hiyo imeshinda imeibuka ya kwanza katika vipengele saba vya umri kati ya 16 za mashindano hayo na kuendelea kutamba nchini katika mchezo huo.

Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha timu saba, waogeleaji wa timu hiyo, Ellie Mramba alikuwa wa kwanza kwa upande wa miaka chini ya sita (U-6 wasichana) kwa kupata pointi 75 huku Sebastian Carpintero alikuwa wa kwanza kwa wavulana wa miaka 7 kwa kupata pointi 112.

Riona Muriithi naye alikuwa wa kwanza kwa upande wa wasichana wa miaka 8 kwa kupata pointi 150, huku Maia Tumiotto akiongoza kwa waogeleaji wenye umri wa miaka 11 wasichana kwa kupata pointi 200 katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na  Spice 4G Communication Unlimited, benki ya CRDB, Dow Elef  International, Davis & Shirtliff, Sea Cliff Hotel, DSTV, American Garde na Sports Arena.

Wadhamini wengine ni Maurel & Orom Tanzania, Warere, Best Western, Makini Studios, Food Lovers Market, UTT AMIS, Renault, CMC Formula, Print Galore, Branoz Collection, Codesh, Coca Cola, Pesi, Emmanuel Edward, The Slip Way Bookshop, Moments by Design, Olive, The Cooking Club, Nzito Shop, Ngozi,Moyo, Coletta na Mothi Mahal.

Marin DE Villard wa klabu hiyo pia alishika nafasi ya kwanza kwa watoto wenye umri wa miaka 11 wavulana na Celina Itatiro  huku akiwa wa kwanza upande wa wasichana wenye umri wa miaka 13 kwa kupata pointi 200 na Joshua Bruns alishinda kwa wavulana wa miaka hiyo kwa kupata pointi 185.

Klabu ya Taliss imeshika nafasi ya pili baada ya kushinda vipengele vinne kupitia Natalia Ladha aliyeshinda  kwa wasichana wenye umri wa miaka 9, Daniella Lamont aliyeshinda kupitia wasichana wenye umri wa miaka 10, Amani Doggart (wasichana miaka 12) na Oliver Mclntosh aliyeshinda kwa wasichana wenye umri wa miaka 12.

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na klabu inayokuja juu katika mchezo huo hapa nchini, Bluefins kwa kushinda vipengele vitatu. Waogeleaji walioipaisha klabu hiyo ni Aminaz Kachra aliyeshinda kwa wasichana wenye umri wa miaka 7 kwa kupata pointi 140, Ralph Sereki (wavulana miaka 8, pointi 165) na Aravid Raghavendran aliyejikusanyia pointi 176 kwa wavulana wa miaka 10.

Klabu ya Wahoo ya Zanzibar alishika nafasi ya nne kupitia kwa Ellis Anderson aliyepata pointi 165 kwa waogeleaji wa miaka 9 wavulana huku klabu ya Champions Rise ikishika nafasi ya tano kwa kushinda kipengele kimoja cha wavulana chini ya miaka 6 kupitia William Sereki aliyepata pointi 75.

Mwanza Swim Club na Kennedy House hazikuweza kushinda vipengele vyovyote vya jumla kwa waogeaji mmoja mmoja. 

Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro alisema kuwa siri ya mafanikio yao imetokana na moyo wa kujituma na ushirikiano baina ya wazazi, makocha na uongozi wa klabu.
“Ni faraja kwetu, kwa sasa tunafurahia matunda ya mafanikio, tumepitia misuko suko kibao, kama si moyo wa uvumilivu, leo tusingekuwa hapa, wachezaji wetu wengi walihama, tuaanza upya na kufikia matunda haya,” alisema Inviolata.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.