Habari za Punde

WATANZANIA WASISITIZWA KUTUMIA MADINI JOTO.

 Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Bw.Suleiman Jaffo aliyesimama akiongea na wazalishaji chumvi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania hawapo pichani wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wazalishaji chumvi uliofanyika jijini Dar es salaam katikati ni Mkrugenzi Msaidizi wa masuala ya Kinga Wizara ya afya Bw. Vicent Assey.
Mkrugenzi Msaidizi wa masuala ya Kinga Wizara ya afya Bw. Vicent Assey akiongea na wazalishaji chumvi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania hawapo pichani wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wazalishaji chumvi uliofanyika jijini Dar es salaam kulia aliyekaa ni Mkrugenzi wa  Mafunzo wa  maendeleo ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle.
Wazalishaji chumvi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wakimsikiliza Mkrugenzi wa  Mafunzo wa  maendeleo ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle hayupo pichani wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wazalishaji chumvi uliofanyika jijini Dar es salaam. Picha Na Ally Daud-Maelezo.
*******************************************************
Na Ally Daud-MAELEZO
WATANZANIA wamesisitizwa kutumia chumvi yenye madini joto kwa wingi ili kuepuka madhara yatokanayo na ukosefu wa madini hayo kwenye mwili wa binadamu kwa ukuaji bora hasa watoto.

Hayo yamesemwa na Mkrugenzi wa  Mafunzo wa  maendeleo ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa wazalishaji chumvi uliofanyika jijini Dar es salaam.

“Asilimia 63 ndio watanzania wanaotumia chumvi yenye madini joto hivyo tunawahasa wananchi waweze kutumia madini hayo kwani usipotumia  yanaleta mapungufu mengi kwa binadamu na madhara yake ni mtoto akizaliwa anakua njiti” alisema Dkt. Gowelle.

Aidha Dkt. Gowelle amesema kuwa Serikali imekusudia kuhakikisha wananchi zaidi ya asilimi 90 wanatumia chumvi yenye madini joto hadi kufikia 2020 ili kuepuka kizazi cha watoto walemavu , wadumavu ,utindio wa ubongo na wenye utapiamlo kutokana na ukosefu wa madini hayo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Bw.Suleiman Jaffo amesema kuwa wapo tayari kuwapigani na kuwasaidia wazalishaji wa chumvi katika kutatua changamoto zao kwenye uzalishaji wa chumvi zenye madini joto.

Aidha Bw. Jaffo alisema kuwa katika kuhakikisha kuinua uchumi wa nchi kupitia viwanda ni lazima itazame na washalishaji wa bidhaa zingine hasa uzalishaji wa chumvi ili kupanua wigo wa masoko ndani na nje ya nchi.Naye Mkrugenzi Msaidizi wa masuala ya Kinga Wizara ya afya Bw. Vicent Assey amesema kuwa watanzania hawana budi kutumia chumvi zenuye madini joto ili kuondoa kizazi chenye matatizo ya kiafya.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.