Habari za Punde

WAZIRI MUHONGO AIPONGEZA KAMPUNI YA ACACIA KWA KUWA KAMPUNI YA KWANZA YA MADINI KUWA NA HATI FUNGANI

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (kulia), na Makamu wa Rais wa Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (anayeshughulikia kampuni), Bw. Deo Mwanyika, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa hati fungani makao makuuya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Acacia imekuwa kampuni ya kwanza ya uchimbaji madini nchini, kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010 inayotaka kila kampuni kuwasilisha mpango wake wa ukarabati wa mzingira na kuweka bond fedha pindi shughuli za uchimbaji zinapokoma. Wanaoshuhudia ni wanasheria wa Wizara na kampuni ya Acacia
**********************************
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa NishatinaMadini, Profesa Sospeter Muhongo, ameipongeza kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, kwakuwa kampuniya kwanza ya madini kusaini mkataba wa hati fungani kwa migodi yote inayomilikiwa na kampuni hiyo ya jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 41.

Waziri aliyasema hayo hivi karibuni baada ya kusaini mkataba huo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapoWaziri Muhongo alisaini kwaniaba ya Serikali, na Makamu wa Rais wa Acacia ,Bw. Deo Mwanyika alisaini kwa niaba ya migodi ya Bulyanhulu, Pangea (Buzwagi) na North Mara.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
“Nimetaarifiwa kwamba Acacia ndio kampuni ya kwanza ya uchimbaji madini kutekeleza kipengele hiki cha sheria hii ya Madini ya mwaka 2010, napenda niwapongeze sana kwa hatua mliyofikia yakutoa hakikisho la kukarabati mazingira kwenye migodi yenu pindi mtakapositisha shughuli za uchimbaji.” Alisema Profesa Muhongo, mara baada ya kusaini mkataba huo.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Migodi nchini, (Acting Chief Inspector of Mine), Mhandisi Noel Baraka, alisema, nijukumu la kisheria kwa migodi yote nchini, ya kati na mikubwa kuandaa mpango wa kufunga mgodi ambao shughuli hiyo inasimamiwa na kamati ya kitaifa ya kusimamia shughuli za ufungaji migodi (National Mine Closure Committee). 

Kamati hiyo inaundwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishatina Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira, (NEMC), Wizara ya Maliasili na Utalii , Wizara ya Maji na Umwagiliaji, National Land Use Planning Commission, viongozi wa Serikali ya mkoa na Wilaya ulipo mgodi husika. 

Mhandisi Baraka alifafanua kuwa Kampuni ya Acacia, iliandaa mipango ya ukarabati wa mazingira pindi shughuli za uchimbaji zitakaposimama na gharama zinazohusiana na ukarabati huo wamigodi yake mitatu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara. 

“Mpango huo na gharama zake ulipitiwa na kamati ya kitaifa ya ufungaji migodi na kuridhishwa na baada ya kuridhishwa ulipitishwa ambapo leo ni hatua ya mwisho ambapo Waziri wa Nishati na Madini, kwaniaba ya Serikali na kiongozi wa Acacia, kwaniaba ya makampuni tanzu wanatia saini mkataba huo.” Alisema Mhandisi Baraka na kuongeza, 

“Chini yamkatabahuu, dhamana (bonds) ya gharama za ukarabati kwa mgodi wa Bulyanhulu, ni Dolaza Kimarekani 3,287,714, Mgodiwa North Mara ni Dola za Kimarekani 19,164,344 na Mgodi wa Buzwagi ni Dola za Kimarekani 18.628,489.” Alifafanua 

“Sheria hii, kampu ni ya uchimbaji madini inapaswa kuweka hati fungani (rehabilitation bonds) kwenye kampuni ya bima au benki, ili shughuli za uchimbahji zinapo koma kwa sababu yoyote ile, basi fedha hizo ziweze kutumika kukarabati mazingira ya eneo la shughuli ya uchimbaji nakuyarejesha katika hali bora na salama.” Alisisitiza. 

Kwaupande wake, Mshauri Mkuu wa Mazingira wa Kampuni ya Acacia, Bi. Rebecca Stephen, alisema kampuni yake imefurahi sana kufikia hatua hiyo ya kusaini mkataba huo, kwani ni hakikisho kwamba fedha tayari zimetengwa kwaajili ya shughuli hiyo. 

“Kazi hii ilikuwa na mchakato mrefu uliochukua takribani miaka miwili, na ulianza kwa kuandaa mpango wa ufungaji mgodi na gharama zake, na kupitiwa na Wizara na kamati nzima na kupitishwa.” Alisema 

Alisema Kampuni ya Acacia katika utekelezaji wa shughuli zake, inazingatia siku zote kutii sheria za nchi na tukio la leo nimoja ya vielelezo, alisema Bi. Rebeca. 

“Sheriayamadini ya 2010 inahitaji kuwepo na hakikisho kutoka kwetu ya namna gani tutakarabati mazingira pindi shughuli za uchimbaji zitakaposimama na kuhakikisha pesa za kufanya ukarabati huo zipo,” alisema na kuongeza Acacia imetekeleza hiyo sheria tukiwa ndio kampuni ya kwanza kufikia hatua hii, alisema Bi. Rebecca. 

Alimalizia kwa kusema, fedha kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 41kwaajili ya migodi yote mitatu tayari tumeweka dhamana kwenye kampuni ya bima ya Metropolitan Tanzania Insurance Company Limited, na kusisitiza kuwa muda wowote fedha hizo zikihitajika zitapatikana.” Alifafanua.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (kulia), na Makamu wa Rais wa Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (anayeshughulikia kampuni), Bw. DFeo Mwanyika, wakitia saini mkataba wa hati fungani makao makuuya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Acacia imekuwa kampuni ya kwanza ya uchimbaji madini nchini, kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010 inayotaka kila kampuni kuwasilisha mpango wake wa ukarabati mzingira na kuweka bondi fedha pindi shughuli za uchimbaji zinapokoma.
Profesac Muhongo, (kulia), akimsikiliza Bw. Mwanyika mwanzoni mwa hafla hiyo ya kutia saini, mkataba wa hati fungani.
Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Migodi nchini, (Acting Chief Inspector of Mine), Mhandisi Noel Baraka(katikati),akielezea mchakato mzima ulivyokwenda na kukamilika
Waziri Muhongo (kushoto), akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo
Makamu wa Rais wa Acacia, Bw. Deo Mwanyika, (kulia) na Mshauri Mkuu wa Mazingira wa kampuni hiyo, Bi. Rebeca Stephene, wakipitia nyaraka hizo kabla ya kusaini
Makamu wa Rais wa Acacia, Bw. Deo Mwanyika, (kulia) na Mshauri Mkuu wa Mazingira wa kampuni hiyo, Bi. Rebeca Stephene, wakipitia nyaraka hizo kabla ya kusaini
Waziri Muhongo (kulia), akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.