Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE ATOA TUZO WA WATUMISHI WA TKU

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikabidhi cheti cha utumishi wa muda mrefu na uliotukuka kwa mmoja wa watumishi wa zamani wa iliyokuwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi, Bibi Fatuma Bakari, Desemba 7, 2016.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na watumishi wa Tume (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumwaga Kamishna wa Tume aliyemalimaliza muda wake na kutoa tuzo kwa watumishi wa zamani wa TKU. Hafla hiyo ilifanyika Desemba 7, 2016 makao makuu ya ofisi za THBUB, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.
**********************************
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe aliongoza hafla fupi ya utoaji wa tuzo na vyeti kwa viongozi na watumishi wa iliyokuwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU). Hafla hiyo iliyoambatana na kumwaga Kamishna wa Tume aliyemaliza muda wake, Mhe. Ali Rajab ilifanyika Makao Makuu ya Ofisi za Tume, mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watumishi wa taasisi hiyo na wageni wachache waalikwa.
Mgeni Rasmi, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikabidhi tuzo ya kutambua utumishi uliotukuka na jitihada za kipekee za kukuza masuala ya uchunguzi wa malalamiko ya wananchi kuhusu matumizi mabaya ya madaraka barani Afrika iliyotolewa na AOMA kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa TKU, marehemu Chifu Erasto Mang’enya. Tuzo hiyo ilipokelewa na mtoto wa marehemu Chifu Mang’enya, Bwana Stewart Mang’enya (pichani).
Bwana Stewart Mang’enya akionesha cheti na tuzo alivyopokea kwa niaba ya familia ya Marehemu, Chifu Erasto Mang’enya huku Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akishangilia. Wengine katika picha (kutoka kulia) ni: Mhe. Bahame Tom Nyanduga, Bibi Mary Massay (Katibu Mtendaji wa THBUB) na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Iddi Ramadhani Mapuri.
Bwana Stewart Mang’enya akionesha cheti na tuzo alivyopokea kwa niaba ya famili ya aliyekuwa Mwenyekiti Mwanzilishi wa iliyokuwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi, Marehemu Chifu Erasto Mang’enya. Mwenyekiti huyo wa kwanza alihudumu vipindi viwili 1965 hadi 1970 na baadaye tena 1972 hadi 1973.
Bwana Emmanuel Ndosi akimpongeza na kumvisha taji mmoja wa watumishi wa iliyokuwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi, Bi. Aziza, huku watumishi wengine wakishindwa kuzuia hisia za furaha yao.
Mhe. Ali Rajab akiwa katika picha ya pamoja na mkewe na watoto wao muda mfupi baada ya Mhe. Rajab na mkewe kuzawadiwa zawadi mbalimbali na jumuiya ya THBUB Desemba 7, mwaka huu. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mwenye tai nyekundu) na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Nyanduga (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa zamani wa iliyokuwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) mara baada ya kupewa vyeti vya utumishi uliotukuka na wa muda mrefu katika hafla fupi iliyofanyika Desemba 7, 2016 makao makuu ya ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Bwana Stewart Erasto Mang’enya (wa tatu kushoto) alipokea tuzo na cheti kwa niaba ya marehemu Baba yake, Chifu Erasto Mang’enya ambaye alikuwa Mwenyekiti Mwanzilishi wa TKU. Tuzo hiyo ilitolewa na Jumuiya ya taasisi za Uchunguzi wa Malalamiko ya Wananchi na Wapatanishi Barani Afrika (African Ombudsman and Mediators Association – AOMA) na kupokelewa na Mhe. Nyanduga katika mkutano wa tano wa AOMA uliofanyika Novemba 4, 2016 mjini Durban, Afrika Kusini. Picha zote na Mbaraka Kambona na Getrude Alex

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.