Habari za Punde

WIZARA YA AFYA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOIKUMBA SEKTA ZA AFYA NCHINI

Na Ally Daud –MAELEZO
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto wamejidhatiti kutatua changamoto zinazoikumba sekta za afya nchini ili kutengeneza Taifa lenye wananchi imara kwa maendeleo ya jamii na uchumi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa kutathimini nakurekebisha Sera ya Afya uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

“Katika mkutano huu tumeadhimia kuongeza bajeti ya dawa nchini kutoka milioni 31 mpaka kufikia milioni 231 ambazo zitachangia kuondoa uhaba ambao umejitogeza hivi karibuni”Alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa katika mkutano huo wanatarajia kupata njia za kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba Sekta ya afya nchini.

Kwa Mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa sekta ya Afya inaupungufu wa watumishi kwa asilimia 49 hivyo kunauhitaji mkubwa wa watumishi katika sekta hiyo ambapo watahitajika ili kuimarisha huduma bora.

Amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kupata kinga juu ya magonjwa ya sioambukizwa ikiwemo kisukari, Magonjwa ya moyo na shinikizo la damu ambapo watazindua kampeni ya mazoezi ya viungo Desema 17 mwaka huu Jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha zahanati zote za serikali zinatumia mashine za Kieletroniki katika kukusanya mapato ya sekta za afya ili kuboresha Huduma.

Wakati huo huo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alipokea msaada wa magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) 10 kwa ajili ya hospitali zaTanzania kutoka ubalozi wa Qatar nchini.
Akipokea magari hayo Waziri Ummy amesema kuwa magari hayo yatasambazwa katika hospitali za rufaa ilikusaidia kupunguza idadi ya vifo vya wagonjwa wanaocheleweshwa kutokana na kukosa usafiri wakuwahishwa kwenye hospitali nyingine.

Aidha Waziri ummy alibainisha hospitali zitakazopata magari hayo ni Mombotanga, Benjamini Mkapa Mbeya, Taasisi ya Jakaya kikwete Muhimbili, Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Dodoma na Ruvuma, hospitali ya Kigamboni na NzegaTabora.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.