Habari za Punde

YANGA YAANZA MZUNGUKO WA PILI KWA KUWACHEZESHA KWATA MAAFANDE WA JKT RUVU 3-0Watetezi wa Ligi Kuu Bara timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam, leo wameanza vyema mzunguko wa pili na wa lala salama wa Ligi Kuu bara kwakuwachezesha kwata maafande wa JKT Ruvu waliokubari kichapo cha mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini jioni ya leo.

Alikuwa ni Deus Kaseke aliyesababisha hekaheka zabao la kwanza na kusababisha beki wa JKT Ruvu, Michael Aidan, kujifunga katika dakika ya 38 kipindi cha kwanza, huku mabao mawili yote yakifungwa na winga mwenye mbio Simon Msuva.
Kwa ushindi huo sasa Yanga wamerejea kileleni wakiongoza ligi hiyo wakiwa na Pointi 36 wakiwazidi pointi 1 watani wao Simba wenye Pointi 35, huku wao wakishuka dimbani kesho mjini Mtwara kukipiga na Ndanda Fc.

MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZA LEO NI:-
Mbeya City 0 - Kagera Sugar 0
Toto African 0 - Mwadui Fc 1
Ruvu Shooting 1 - Mtibwa Sugar 1

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.