Habari za Punde

ASHA BARAKA AMUWAKIA CHOKI KUVUNJA MKATABA NA TWANGA

Na Mwandishi Wetu, Dar
Mkurugenzi wa kampuni ya ASETt Entertiment inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, amekuja juu mara baada ya kusikia habari kuwa mwanamuziki kinara wa bendi hiyo Ali Choki anataka kuondoka.

Asha Baraka ambaye amempigia simu ripota wa Globu ya Jamii mara baada ya kuandikwa habari hizo na kusema: 
“Nasema hivi... (Ali) Choki hawezi kuondoka Twanga Pepeta kwa kuwa alisaini mwenyewe mkataba wa miaka mitatu na mkataba huo unamalizika mwaka 2018. Sasa huyo anayemtaka Choki asubiri wakati ufike ndio aanze kumshawishi...” amesema Asha Baraka.

Hata hivyo Asha Baraka marufu kama "Iron Lady" (mama wa chuma) alipoulizwa juu ya mtu anayehitaji kuvunja mkataba anatakiwa kulipa kiasi gani cha fedha, amesema: 

"Mimi nipo na mwanamuziki kwa mkataba wa miaka mitatu. Sasa huyo anayetaka kuvunja mkataba wangu na Choki mwambie siko tayari kuzungumzia swala la kuvunja mkataba. 

Kwa sasa mimi nipo kwa ajili ya kuimarisha bendi na sio kubomoa bendi..."

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.