Habari za Punde

AZAM FC WAENDELEZA UBABE KWA MNYAMA SIMBA WAMPA 1-0 UWANJA WA TAIFA

 Beki wa Azam Fc, Gadiel Michael (kulia) akichuana kuwania mpira na winga wa Simba Jamal Mnyate wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Azam Fc wameibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Nahodha John Bocco katika dakika ya 70, akifanyia kazi makosa ya beki Method Mwanjali aliyekosea kuondoa mpira huo wa hatari katika eneo lake na kupitiwa na John Bocco aliyeambaa nao hadi kumchungulia Kipa wa Simba, Daniel Agyei.
 Kipa Daniel Agyei, akiuangalia mpira uliokuwa ukielekea langoni kwake na kutoka nje uliopigwa na Joseph Mahundi katika kipindi cha kwanza.
 Joseph Mahundi akijikunja kupiga shuti langoni mwa Simba
 Beki wa Simba, Mohammed Hussein (kulia) akichuana na Mudathir Yahya...
 Mashabiki wa Azam wakishangilia
 Hayahaya Mohammed wa Azam Fc (kushoto) akichuana na Nahodha wa Simba, Jonas Mkude
 Hayahaya Mohammed wa Azam Fc (kushoto) akichuana na Nahodha wa Simba, Jonas Mkude
 Frank Domayo akichuana na wachezaji wa Simba
 Bocco akimiliki mpira na kujaribu kumchambua kipa wa Simba bila mafanikio
 Joseph Mahundi akiwania mpira na Muzamir Yassir
 Bocco akimiliki mpira mbele ya mabeki wa Simba
 Kipa wa Simba akimfinya John Bocco
 Hapa ilikuwa ni mshike mshike kati ya Gadiel na Mnyate
Hapa Hupiti ni roba tuuuuuuu
 Weee tuliaaaaaaaaaaaaaa
 Roba takatifu
 Mashabiki wa Simba wakinywea kimyaaaaaaa
 Hakijaeleweka
 Kimyaaaaaaaaaa
KIKOSI CHA SIMBA: 
Jonas Mkude, Daniel Agyei, Javier Bukungu, Mohammed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjale, Juma Luizio, Muzamiru Yassin, Pastory Athanas, Said Ndemla na Jamal Mnyate.

KIKOSI CHA AKIBA:
Peter Manyika, Vicent Costa, Novalt Lufunga, Laudit Mavugo, James Kotei, Ibrahim Ajib na Shizza Kichuya.
KIKOSI CHA AZAM FC:
John Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Mihcael, Agrey Mirris, Yakub Mohammed, Stephan Kingue, Himid Mao, Frank Domayo, Ramadhan Singano na Joseph Mahundi

BENCHI LA AKIBA:
Metacha Mnata, David Mwantika, Abdallah Kheri, Shaban Iddi, Masoud Abdallah, Mudathir Yahya na Yahaya Mohammed

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.