Habari za Punde

AZAM SPORTS FEDERATION CUP KUENDELEA KESHO KWA MECHI MOJA

Mchezo mmoja wa Azam Sports Federation Cup kati ya Mshikamano na African Lyon – zote za Dar es Salaam unatarajiwa kufanyika kesho Jumatano Februari mosi, 2017 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ni pekee uliobaki kuchezwa hatua/Raundi ya Tano ambayo ilishirikisha timu 32. Tayari timu 15 zilipatikana na kupatikana na mshindi wa mchezo wa kesho, kutatimiza timu 16 bora.
Timu hizo zitakwenda kucheza hatua/raundi ya sita mwishoni wa Februari – kuanzia Februari 25, 26, 27 na 28.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.