Habari za Punde

BALOZI IDDI ATEMBELEA KUKAGUA MRADI WA TASAF KUZUIA MAJI YA BAHARI ZANZIBAR

Mhandisi wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Pemba, Talib Bakari (kushoto) akimuonesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Tuta la udongo lililomwagwa kuzuia Maji ya Bahari linaloendelea kujengwa kwenye Bonde la Kidau Ndagoni kupiti Mradi wa Tasaf, wakati Balozi Iddi alipotembelea kukagua mradi huo.
Balozi Seif akiangalia eneo la Bonde la Kidau ambalo limeathirika kwa maji ya Mvua akiambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi (kulia kwake). Kushoto kwa Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed. Picha na – OMPR – ZNZ.
*************************************************
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema miradi
ya Kijamii inayoendeshwa kupitia Mfuko wa wa Maendeleo ya Jamii
Tanaznia {TASAF } inalazimika kuibiliwa na wananchi wenyewe
katika maeneo yao kwa vile wao ndio wanaoelewa mazingira
yanayowazunguuka.
Alisema Serikali Kuu kazi yake kubwa ni kuongeza nguvu za uwezeshaji
katika kuona miradi hiyo inaimarika na kukua kwa lengo la kuwaondoshea
ukali wa maisha Wananchi wake katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya
Unguja na Pemba.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo akiwa katika ziara ya siku Tatu
Kisiwani Pemba kuangalia miradi ya Maendeleo wakati alipokagua miradi
ya Tasaf katika Bonde la Kidau Ndagoni kuona maendeleo ya ujenzi wa
Tuta la kuzuia maji ya Bahari yanayoathiri wakulima wa bonde hilo.
Alisema yapo maendeleo makubwa yaliyopatikana tokea kuanzishwa kwa
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} hasa katika kuzisaidia
Kaya Maskini zilizozongwa na ukali wa maisha ziwe na miundombinu ya
kujiendesha Kimaisha kupitia miradi wanayoianzisha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi na wakulima
hao wa Bonde la Kidau pamoja na wale wote wanaopata huduma kupitia
mfuko wa Tasaf kutokana na juhudi kubwa wanazozichukuwa katika
kuimarisha miradi yao ikiwemo ile ya sekta ya kilimo iliyokuwa tegemeo
kubwa la wananchi wa Zanzibar kwa zaidi ya asilimia 8%.
Akitoa ufafanuzi wa kitaalamu wa ujenzi wa Tuta hilo la kuzuia maji ya
bahari katika Bonde la Kidau Ndagoni Mhandisi wa Wizra ya Kilimo,
Maliasili, Mifugo na Uvuvi nd. Talib Bakari alisema zaidi ya Eka 33
kwenye Bonde hilo zimekuwa zikiingia Maji ya Bahari.
Nd. Bakari alisema hali hiyo imewafanya Wakulima wapatao 92
wameathirika na tatizo hilo lililopelekea kukosa kuendelea na harakati
zao za kilimo cha Munga pamoja na mazao mengine ya nafaka.
Mhandisi Bakari alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba
athari hiyo iliyokuwa kero kwa wakulima hao na pia kuchangia uharibifu
wa mazingira ilipeklekea wananchi na Wakulima hao kuwamua ujenzi wa
Tuta ili kunusuru hali hiyo.
Alisema ujenzi wa Tuta hilo la kuzuia maji ya Bahari ambao kwa sasa
umeshafikia asilimia 90% unaotarajiwa kuchukuwa siku 45 hadi
kukamilika kwake utaweza kuwafaidisha Wakulima 92.
Alifafanua kwamba gharama za ujenzi wa Tuta hilo utafikia jumla ya
shilingi Milioni 37,000,000/- ambazo kati ya hizo Milioni 30,000,000/-
zimewagusa Wananchi wenyewe wa Kaya Maskini na zilizobakia milioni 7
zimepangwa kuhudumia wafanyakazi ambao wengine ni miongoni mwao.
Mapema Mkulima Maisuri Omar Suleiman kwa niaba ya wakulima wenzake wa
Bonde hilo la Kidau Ndagoni wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa uamuzi wake wa kuwapatia mradi wa Tasaf ambao wameueleza
kuwa umeleta ukombozi mkubwa kwao.
Mkulima Maisuri alisema wakulima na wananchi wa Vijiji vilivyo jitrani
na Bonde hilo wamepata faraja kubwa kupitia Mfuko wa Tasaf jambo
ambalo kwa kiasi kuikubwa wamefanikiwa kupunguza ukali wa maisha na
kujiongezea kipato kinachoashiria kusaidia familia zao.
Hata hivyo Mkulima Maisuni kwa niaba ya wakulima na wananchi wenzake
wameiomba Serikali Kuu kufikiria kuwaongezea uwezeshaji zaidi kwa
ajili ya kuendesha miradi mengine ya maendeleo na kiuchumi ili kufikia
malengo yao waliyojipangia.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.