Habari za Punde

BALOZI WA TANZANIA UINGEREZA DKT. ASHA ROSE-MIGIRO KUTEMBELEA LEICESTER

Jumuia ya Watanzania Leicester, UK inapenda kuwaarifu Watanzania, wenye nasaba na Tanzania pamoja na marafiki wa Tanzania kuwa Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Uingereza, Dokta Asha Rose-Migiro (katika picha ya maktaba akiwa na mdau Freddy Macha, London) atafanya ziara katika mji wa Leicester kwa utaratibu ufuatao: 
SIKU: JUMAMOSI
Tarehe 04.02.2017. 
Ratiba itaanza kwa Mheshimiwa Balozi kutembelea shughuli mbali mbali za kimaendeleo za wajasiriamali wa kitanzania hapa Leicester. 
Saa Nane Kamili mchana (2.00pm) Mheshimiwa Balozi atafanya mazungumzo na Watanzania, marafiki na wenye nasaba na Tanzania katika ukumbi huu: 
ST MATTHEWS NEIGHBOURHOOD CENTRE,
10 MALABAR ROAD,
LEICESTER UK LE1 2PD 
Tunatumia fursa hii kukualikeni nyote katika kikao hicho kitachokuwa na umuhimu wa pekee. Masuala mengi muhimu yatafafanuliwa na Mheshimiwa Balozi, yakiwemo: 
- Ufafanuzi na maelezo kuhusu Uraia pacha (dual citizenship)
- Umiliki ardhi kwa diaspora
Pamoja na mengi mengine. 
Tafadhali tufike bila kukosa.
Tafadhali tuwaarifu na wenzetu.
Shukran.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.