Habari za Punde

BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUKUZA UCHUMI

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), walipokutana kwaajili ya mazungumzo Makao makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam. Wanao shuhudia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anaye hudumia nchi za Tanzania, Malawi, Burundi, Bella Bird na Msaidizi wa Waziri wa Fedha na Mipango, Bw. Edwin Makamba (aliyesimama)
Baadhi ya Watendaji wakuu wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakiwa katika Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop ( hawapo Pichani), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Ujumbe wa Tanzania na Benki ya Dunia, ukiwa katika kikao kilichojadili masuala mbalimbali yanayogusa Serikali na Benki hiyo, wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, pamoja na Mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango,Jijini Dar es salaam,
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa Pili kutoka kulia) akisisitiza jambo wakati wa alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia ukanda wa Afrika Bw. Makhtar Diop, makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar salaam.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wizara na Taasisi zake baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yake na mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Makao Makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiagana na Mgeni wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, mara baada ya kumalizika kwamazungumzo kati yao, ambapo Benki hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia Mikopo yenye mashari Nafuu kwaajili ya miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii. Picha na Ben Mwaipaja - WFM

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.