Habari za Punde

CHEKI HAPA MABAO 6 YA YANGA DHIDI YA JAMHURI FC, KOMBE LA MAPINDUZI

TIMU Kongwe za Tanzania Bara,Yanga, Simba na Azam zimeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar baada ya kila moja kuibuka na ushindi.Simba wao walianza vyema kwa kuichapa Taifa Jang’ombe mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar. 

Huku Azam Fc wao wakiibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Zima Moto katika mchezo uliopigwa majira ya saa kumi jioni ya leo kwenye Uwanja wa Aman.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara wao wamefungua pazia lamichuano hiyo usiku huu kwa kuwachabanga bila huuma mabao 6-0 Jamhuri fc katika uwanja wa Amani.

Mabao hao yalifungwa na Simon Msuva 2, Donald Ngoma 3, Thaban Kamusoko 1 na Juma Mahadhi 1.

Kwa ushindi huo unaifanya Yanga kuongoza Kundi B wakiwa na Pointi 3 sawa na Azam Fc,lakini wakiwa na mabao mengi ya kufunga.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.