Habari za Punde

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA BANDARI

Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wakiendelea na Kikao.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani (Mb) (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam mapema leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hawa Ghasia(Mb). Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza shughuli zake hii leo ambapo katika wiki hii takribani Kamati za Kisekta 12 zitakuwa zikifanya ziara za kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini kabla ya kurejea Mjini Dodoma kwa ajili kuendelea na vikao vyake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akimueleza jambo Kaimu Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali wakati wa ziara hiyo.
Kaimu Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati wa ziara hiyo. 
Picha na Ofisi ya Bunge

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.