Habari za Punde

KIKOSI CHA MBEYA CITY CHATAMBA KUIBUKA NA POINTI TATU KWA WAPINZANI WAO PRISONS

BAADA ya ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Kabela City Fc ya Shinyanga kwenye kombe la FA hapo jana, kikosi cha Mbeya City Fc leo kimeanza mazoezi kujindaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prison uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza na mtandao huu Kocha msaidizi wa kikosi hicho, Mohamed Kijusoalisema kuwa maandalizi kuelekea mchezo huo wa jumamosi yanaendelea vizuri na wachezaji wote wako kwenye hali nzuri, kinachofanyika sasa ni kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kombe la FA licha ya kupatikana kwa ushindi wa bao 2-0.
Tunashukuru Mungu kwa sababu tulipata matokeo kwenye mchezo wa kombe la FA hapo jana licha ya mchezo kuwa mgumu, tuko mazoezini hivi sasa kurekebisha makosa yote yalitokea hii ni sehemu ya maandalizi yetu kuelekea mchezo ujao,kwa mujibu wa daktari vijan wangu wote wako fiti, naiheshimu Tanzania Prison ni timu nzuri huwezi kuibeza kwa namna yoyote, ni wazi mchezo wa jumamosi utakuwa mgumu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.