Habari za Punde

MABONDIA RAMADHAN SHAURI, MESHACK MWANKEMWA WATAMBULISHWA KUZICHAPA FEB 5 UWANJA WA NDANI WA TAIFA DAR

Muwakilishi wa Kamisheni ya mchezo wa ngumi nchini (TPBC), Joe Anae (kati) akiwatambulisha Mabondia Ramadhan Shauri (kulia) na Meshark Mwankemwa (kushoto) watakaozichapa Februari 5, 2017 katika uwanja wa ndani wa Taifa, Jijini Dar es salaam ikiwa ni mpambano wa kuwania mkanda wa Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (66.7kg Welterweight). ulioandaliwa na Promota wa mchezo wa ngumi "Masumbwi" wa muda mrefu, Sadick Kinyogoli kupitia Kampuni yake ya SADICK & CO. LTD, Mambondia hao wametambiana kwa kila mmoja kuonyesha nia ya kumshinda mwenzake katika mpambano huo. Kabla ya pambano la Mabondia Ramadhan Shauri na Meshark Mwankemwa, kutakuwa na mapambano ya utangulizi yapatayo saba, likiwepo lile lililosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa mchezo wa masumbwi la Mabondia Mohamed Matumla na Mfaume Mfaume (62 KG LIGHT weight).
Muwakilishi wa Kamisheni ya mchezo wa ngumi nchini (TPBC), Joe Anae (wa pili kulia) akimkabidhi fedha Bondia Meshark Mwankemwa kwa maandalizi ya mpambano wake dhidi ya Bondia Ramadhan Shauri (kulia).
Muwakilishi wa Kamisheni ya mchezo wa ngumi nchini (TPBC), Joe Anae (katikati) akimkabidhi fedha Bondia Ramadhan Shauri kwa maandalizi ya mpambano wake dhidi ya Bondia Meshark Mwankemwa.
Bondia Ramadhan Shauri akimwaga wino kukubali kuzichapa na Bondia Meshark Mwankemwa
Naye Bondia Meshark Mwankemwa akimwaga wino kukubali kukipiga na Bondia Ramadhan Shauri.
Muwakilishi wa Kamisheni ya mchezo wa ngumi nchini (TPBC), Joe Anae akiwatambulisha Mabondia Mohamed Matumla (kulia) na Mfaume Mfaume.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.