Habari za Punde

MACHINGA WAIFANYIA KAZI KAULI DKT MAGUFULI SOKO LA KARUME

 Pamoja na agizo la Mh. Rais Dkt John Pombe Magufuli, la kutowasumbua wala kuwabughudhi kwa kuwafukuza wafanyabiashara Machinga katika maeneo ya katikati ya miji na pembezoni mwa barabara lakini katika barabara hii ya Karume wafanyabiashara hawa wamezidi kujiachia zaidi kwa kujibegea eneo kubwa kiasi cha kuchukua hadi eneo la njia ya wapita kwa miguu jambo ambalo linawafanya waenda kwa miguu kupita barabara ya magari jambo ambalo ni hatari. 
 Meza za wafanyabiashara zikiwa zimeziba njia ya waenda kwa miguu
 Waenda kwa miguu wakilazimika kupita barabarani kutokana na eneo hilo kuzibwa na meza za wafanyabiashara wa nguo katika Soko hilo la Karume.
 Hakuna njia tena ya waenda kwa miguu eneo hili
 Hii ni hatari, wahusika inabidi kufika eneo hili na kuchukua hatua........

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.