Habari za Punde

MADEREVA WAKANUSHA TAARIFA ZA KUWEPO KWA MGOMO

 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWA) Bw. Shabani Mdemu (kulia) akikanusha taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya mitandao ya kijamii hapa nchini kuwa madereva wamepanga kufanya mgomo mapema mwezi Februari, amesema chama hicho hakijapanga mgomo wowote kama ilivyotangazwa hivyo wananchi wapuuze taarifa hizo kwa kuwa si za kweli. Kushoti ni Msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ridhiwani Wema.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Wasafirishaji  kwa Njia ya Barabara Bw. Salum Abdallah akitoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa za kuwepo kwa mgomo wa madereva kama ilivyoripotiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii na kuliomba Jeshi la Polisi kuchukua hatua kwa wote waliohusika kusambaza taarifa hizo za upotoshaji. Kulia ni Mwenyekiti wa chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWA) Bw. Shabani Mdemu.
Msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ridhiwani Wema akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu taarifa za upotoshaji kuhusu kuwepo kwa mgomo wa madereva zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii. Picha na Frank Mvungi-Maelezo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.