Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA KUSHIRIKI UZINDUZI WA MABASI YA MWENDO KASI-BRT

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, (wa pili kushoto aliyeshika dafu) alipowasili nchini, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa tatu kushoto) ambapo anatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017, na baadaye kufanya mazungunzo na Waziri huyo alasiri.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa na Mgeni wake ambaye ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, wakiwa katika chumba cha kupumzikia wageni maalumu katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi Bi. Bella Bird.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, (kushoto) akinywa maji ya dafu alipowasili nchini, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) ambapo anatarajiwa kuungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika uzinduzi wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi, baada ya mapokezi ya Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.