Habari za Punde

MAREHEMU AMINA ATHUMAN KUZIKWA KIJIJINI KWAO LUSHOTOKatibu wa Kamati ya Maandalizi Kombe la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar, Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athumani, Toufik Majaliwa, alipofika nyumbani kwa jamaa wa marehemu katika mtaa wa kariakoo unguja jana kutoa mkono wa pole akiwa na waandishi wa habari za michezo Zanzibar ZASWA.
************************************Kwa mujibu wa taarifa za msemaji wa familia, Nurdin Ramadhani amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo asubuhi na Boti ya Kampuni ya Azam Marine saa moja asubuhi kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Kijijini kwao Lushoto siku ya kesho Jumanne mchana. 

Mwili wa marehemu utawasili jijini Dar es Salaam saa tatu asubuhi ukitokea Zanzibar baada ya kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam utasafirishwa kuelekea kijiji kwao Wilaya ya Lushoto MkoanoITanga kwa ajili ya mazishi.

Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Ndg Khamis Said akimfariji kaka wa marehemu. Nurdin Ramadhani alipofika katika msiba kutoa pole.


Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Said akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar Zaswa alipofika nyumbani kwa ndugu wa marehemu katika mtaa wa kariakoo zanzibar.


Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar, Mwinyimvua Mnzuki akizungumza na waandishi wa habari kwa kupokea kwa masikitiko kifo cha mwandishi mwezao mrehemu Amani Athuman kilichotokea jana asubuhi katika hopspitali ya mnazi mmoja.


Ndugu wa marehemu wakiwa ma ,ajomzi wakisubiri taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.


Wanafamilia wa marehemu Amina Athumani wakiwa katika msiba huo katika mtaa wa kariakoo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.