Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA MECHI YA KIJITONYAMA UNITED VS MILAMBO FORT EAGLES JANA

 Beki wa Kijitonyama United, John Mwingira, akiruka kumdhibiti mshambuliaji wa Milambo wakati wa mchezo wao wajana wa Ligi uliopigwa kwenye Uwanja wa Makurumla Mwembe Chai jijini Dar es Salaam.Katika mchezo huo Milambo Fort Eagles, waliibuka na ushindi wa mabao 2-1. 

Kijitonyama mpaka sasa wamecheza mechi mbili ambapo ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Mkunguni iliyopigwa katika Uwanja wa Airwing ambayowalitoka sare ya 0-0. 
 Sehemu ya mashabiki wa timu ya Milambo wakifanya yao uwanjani hapo huku wengine wakitishia amani kwa wapinzani wao.
 Na wafanya biashara ya Uji nao hawako nyuma kuchangamkia fursa
 Mijoka wa Kijitonyama Veterans (kulia) akibishana na mashabiki wa Milambo waliokuwa waipita upande wao na kutukana matusi ya nguoni na kutishia amani kwa wapinzani wao.
 Wachezaji wakisalimiana baadaya timu zote kukaguliwa kabla ya kuanza mtanange huo.
 Kikosi cha timu ya Kijitonyama United
Kikosi cha timu ya Milambo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.