Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA YANGA IKISHINDA MABAO 2-0 DHIDI YA MWADUI FC UWANJA WA TAIFA

 Mshambuliaji wa Yanga aliyetokea benchi Obrey Chirwa, akichukua nafasi ya Haruna Niyonzima, leo ameiwezesha Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui Fc katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Amis Tambwe akiwatoka mabeki wa Mwadui Fc


Na Zainab Nyamka, Dar
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara wamefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa  ligi baada ya kutoka na ushindi wa goli 2-0 kwenye mchezo uliofanyika leo katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Obrey Chirwa aliyeingia dakika ya 62 akichukua nafasi ya Haruna Niyonzima alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kuifungia timu yake goli 2 katika dakika ya 69 na 82.
Yanga waliingia uwanja wakitafuta ushindi wa aina yoyote ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu  hizo zilienda mapumziko wakiwa hawajafungana.
Mwadui waliokuwa makini katika safu yao ya ulinzi waliweza kuwadhibiti washambuliaji wa Yanga na kuwafanya kushindwa kupata goli la mapema.
Kila upande walifanya mabadiliko kwa ajili ya kusaka ushindi huo, na baada ya matokeo haya Yanga anaongoza ligi akiwa na alama 46, akifuatiwa na Simba mwenye alama 45 huku Azam akiwa na alama 34.
 Wakishangilia bao la pili la Obrey Chirwa
 KIKOSI CHA YANGA:
Nadir Haroub 'Canavaro' (c), Deogratias Munishi, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani, Justine Zulu, Simon Msuva, Thaban Kamusoko, Amis Tambwe, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke.

BENCHI LA AKIBA: 
Beno David, Oscar Joshua, Said Juma, Yusuf Mhilu, Obrey Chirwa, Emmanuel Martine na Geofrey Mwashiuya
KIKOSI  CHA MWADUI FC:
Iddi Mobby (c), Shaban Kado, Nassoro Cholo, Yassin Mustapha, Malika Ndeule, Hassan Kabunda, Razack Khalfan,Awadh Juma, Paul Nonga, Salim Khamis na Abdallah Seseme 

BENCHI LA AKIBA:
Lucheke Mussa, Salum Kanoni, David Luhende, Shabani Aboma, Meshack Meshack, Jerryson Tegete na Joseph Kimwaga

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.