Habari za Punde

MBEYA CITY WAMSIKITIKIA KIPA WAO WA ZAMANI BURHANI, WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI


Klabu ya Mbeya City fc imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha aliyekuwa mchezaji wake David Burhan kilichotokea usiku kuamkia leo kwenye Hospital ya Bugando jijini Mwanza.
Akizungumza mapema leo Mwenyekiti wa City Mussa Mapunda amesema kuwa, ameshtushwa na taarifa ya kifo cha mchezaji huyo aliyekuwa nguzo kubwa katika mafanikio iliyopata mbeya City tangu ilipanda daraja na kucheza ligi kuu ya Vodacom.
Binafsi nimeshtushwa na taarifa hizo,Burhan alikuwa sehemu ya mafanikio ya kikosi chetu tangu alipojiunga nasi akitokea Prisons,baada ya kuhamia klabu nyingine tulikuwa tukiwasiliana nae mara kwa mara na kutoa mchango wake pale alipoona pana umuhimu wa kufanya hivyo,hatuna namna nyingine ni kumshukuu Mungu kwa sababu yote ni kazi yake na tunamuomba ampumzishe kwa amani ameni.
Kwa niaba ya klabu naomba kutoa salamu za pole kwa familia ndugu,jamaa pamoja na wadua wote wa soka, kwa sasa tunaendelea kufanya mawasilino na wana familia ili kujua taratibu zote na klabu itashiriki mazishi ya mpendwa wetu.
Kwa upande wao wachezaji Hassan Mwasapili na John Kabanda ambao walicheza pamoja na Marehemu David Burhan kwenye kikosi cha City wameeleza kusikitishwa kwao na taarifa za kifo hicho, huku wakikumbuka namna walivyokuwa wakiishi nae wakati wa uhai wake.Audio Player.

''Nimesikitishwa, ni mtu ambaye alikuwa akiniongoza kwenye mambo mengi, alinishauri kuendelea kupambana ili kutimiza malengo niliyonayo, daima nitamkumbuka- Hassan Mwasapili.
Sina la kusema,alikuwa ni kama ndugu yangu kwa namna nilivyoishi nae,ni kazi ya Mungu haina makosa R.I.P David Burhan'' alisema John Kabanda.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.