Habari za Punde

MECHI YA SIMBA VS YANGA YA FEB 18 YASOGEZWA MBELE

Na Asia Gamba, Dar
Mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu  Tanzania Bara wa Watani wa Jadi Simba na Yanga umesogezwa mbele hadi Februari 25, kutoka na Yanga kuwa na mashindano ya kimataifa, ambapo itawawia vigumu kucheza siku hiyo.

Mchezo huo uliotakiwa kufanyika Februari 18, mwaka huu umesogezwa mbele kuwapisha Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu 2015/2016 kumaliza mechi zao dhidi ya Ngaye De Mba ambao utachezwa Februari 10 nchini Comoro na kurudiana Februari 17 katika Uwanja wa Taifa.

Habari kutoka ndani ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba sababu ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni muingiliano na Ratiba ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Kwa sababu hiyo, mchezo wa Simba na Yanga usingeweza kufanyika tena Februari 18 na busara za TFF zimeupeleka hadi Februari 25.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.