Habari za Punde

MKUTANO WA WAZIRI MUHONGO NA KAMATI YA WACHIMBAJI NA WANUNUZI WA JASI NA MAKAA YA MAWE TANZANIA

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza kwenye mkutano na Kamati ya Wachimbaji na Wanunuzi wa Jasi na Makaa ya Mawe Tanzania. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Dangote, nchini Tanzania, Harpreet Duggal akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Devakumar Edwin.
*******************************************
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo hivi karibuni alikutana na wajumbe wa Kamati ya Wazalishaji na Wanunuzi wa Madini ya Jasi na Makaa ya Mawe Nchini katika Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Masuala mbalimbali kuhusiana na biashara ya madini hayo kwa ujumla yalijadiliwa kwa lengo la kuleta tija kwa pande zote na Taifa kwa ujumla.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Wizara ambao wamo ndani ya Kamati husika akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa James Mdoe, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na Makamishna Wasaidizi wa Madini kwenye Kanda zinazozalisha madini husika.
Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati husika, Profesa James Mdoe, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). 
Baadhi ya wajumbe kutoka Kampuni ya Dangote wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Dangote, Devakumar Edwin, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Dangote, nchini Tanzania, Harpreet Duggal. 
Wawakilishi kutoka Kampuni inayochimba Makaa ya Mawe ya Tancoal waliohudhuria mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu, Jim Shedd, Mkuu wa Masoko, Emmanuel Constantinides na Mkurugenzi Mtendaji, Mark McAndrew wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.