Habari za Punde

MWENYEKITI WA CCM MBEYA ALIVYOPIGWA RISASI, POLISI MKOA WA MBEYA KUENDELEA NA MSAKO

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya , Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Emmanuel G. Lukula
*******************************************
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Mafanikio yaliyopatikana katika msako ni kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 23:45hrs katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. EFRAHIM S/O MWAITENDA, [60], mkazi wa Ntembela mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu/watu wasiofahamika akiwa amelala kitandani nyumbani kwake, mbinu ni kukata wavu wa dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi za gololi, nia ni kutaka kuumua. Mhanga amefikishwa Hospitali ya Rufaa na hali yake inaendelea vizuri. Juhudi za kuwatafuta na kuwakamata zinaendelea.

Aidha mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 10:30hrs, katika mpaka wa nchi ya Mlawi na Tanzania Kasumulu Wilayani Kyela, mfanyabiashara ajulikanae kwa jina moja la JAPHET amekamatwa na kikosi maalumu [Task Force ] ya TRA , POLISI na MAAFISA WAKILIMO akiwa anavusha mahidi kwa njia ya panya kutoka nchi jirani ya Malawi bila ya kufuata utaratibu wa sheria za uingizaji chakula nchini. Mahidi hayo yamekamatwa yakiwa kwenye gari moja aina ya canter na mengine yalikuwa yamehifadhiwa kwenye store. 

Wakati wa uchukuaji wa mahidi store kundi la wananchi walijitokeza na walianza kuwazuia maafisa wa TRA kupakia mahindi hayo kwa kile walichodai kuwa wanauziwa mahindi hayo kwa bei rahisi. Kutokana na hali hiyo Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao. 

Hata hivyo hali baada ya muda ilirejea kuwa shwari. Ufuatiliaji wa karibu unaendelea ili kubaini wafanyabiashara wenye tabia kama hiyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL G. LUKULA anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria pia anatoa onyo kwa wafanyabiashara wasiofuata sheria, kanuni na taratibu za kusafirisha bidhaa iwe kutoa au kuingiza kwani mkono wa sheria utawafikia kwani Jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau wengine linaendelea kufanya misako ili kukomesha tabia hiyo. 

Aidha anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
[EMANUEL G. LUKULA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.