Habari za Punde

RAIS DKT. MAGUFULI ATEMBELEA KIJIWE CHAKE NA SHULE YA MSINGI ALIYOSOMA CHATO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati ya wanafunzi) akifurahia pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita, wakati alipotebelea shule hiyo aliyosoma kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la Saba. Rais Dkt. Magufuli amewaasa Wanafunzi hao kusoma kwa bidii huenda Magufuli mwingine akatokea katika shue hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita. Shule hiyo ya Msingi Chato ndiyo Rais Dkt. Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la Saba. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika benchi la kibanda cha kupigia kiwi (Shoe Shine) pamoja na wakazi wengine wa Chato katika eneo maarufu kama Stendi za zamani Chato mkoani Geita. Kibanda hicho cha Kiwi ndicho Rais Dkt. Magufuli alichokuwa akisafishiwa viatu vyake kabla ya kuwa Rais, pia ni sehemu ambayo alikuwa akipenda kukaa na kubadilishana mawazo na wakazi wa Chato wakati akiwa mapumzikoni kipindi cha Nyuma.
Akiwa Kijiweni Chato

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.