Habari za Punde

SHEREHE ZA UFUNGUZI RASMI WA AWAMU YA KWANZA YA MIUNDOMBINU NA UTOAJI HUDUMA YA MABASI YA MWENDO KASI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba kwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam leo Jumatano Januari 25, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wa kwanza kulia wavivuta kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka kadi ya Kieletroniki katika Mashine ya UDART ilikuweza kupita kama ishara ya Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene akimuelekeza jambo katika mashine hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye mashine hizo mara baada ya uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu wakimshangilia Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam leo Jumatano Januari 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop pamoja na viongozi wengine meza kuu wakifurahia nyimbo za msanii Mrisho Mpoto na Banana Zorro kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam leo Jumatano Januari 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop pamoja na viongozi wengine meza kuu wakifurahia nyimbo na kwenda kumtuza msanii Mrisho Mpoto na Banana Zorro kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam leo Jumatano Januari 25, 2017
Mungu ampe nini Msanii Mrisho Mpoto baada ya kuambulia burungutu la noti baada ya kutumbuiza kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam leo Jumatano Januari 25, 2017
************************************************
RAIS MAGUFULI: JENGENI KITUO CHA DALADALA NA KUPAKI MAGARI MADOGO KIMARA MWISHO
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ameagiza kujengwa kituo kikubwa cha kupaki magari na kituo cha daladala ili kuwawezesha wananchi wanaotumia magari binafsi kupaki Kimara mwisho na kutumia usafiri wa mwendokasi ili kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es salaam.
Rais Magufuli ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji wa Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) katika Kituo Kikuu cha Mabasi kilichopo Kariakoo eneo la Gerezani.
“Wito wangu ni kwamba kuna watu wengi wana magari madogo madogo na wanatoka sehemu mbalimbali mpaka kufika kituo cha Kimara mwisho na kuna eneo kubwa pale la hifadhi ya barabara ambalo halihitaji hata kulipa fidia ili kulitumia,wananchi  wanaona adha ya foleni iliyopo lakini hawana sehemu ya kupaki magari yao ili watumie magari ya mwendo kasi,nawaomba mjenge kituo cha magari madogo madogo eneo hili la Kimara ili wananchi hawa wafaidike vyema na mradi huu”, aliongeza Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ametoa wito kujengwa kwa kituo cha mabasi ya daladala katika eneo la Kimara mwisho ili kuwasaidia wananchi wanaofika katika kituo cha magari ya mwendokasi kutopata shida ya kuunganisha magari ya kwenda Mbezi na sehemu nyingine za Jiji kwani watakuwa na kituo rasmi.
Awali akizungumzia mradi huu Rais Magufuli alisema kuwa iliwachukua abiria kusafiri kwa zaidi ya masaa matatu kutoka Kimara mpaka posta lakini kukamilika kwa mradi huu kumesaidia kurahisisha abiria kufika kituo cha Posta kwa kutumia dakika 30 mpaka 40 na hivyo mradi huu kuwa kichocheo kikubwa cha uchumi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huu wa awamu ya kwanza wenye kilometa 20.9 umetumia jumla ya shilingi bilioni 403.5 ambapo Tanzania imechangia bilioni 86.5 na Benki ya Dunia wametukopesha bilioni 317.
Amesema kuwa kukamilika kwa awamu ya kwanza kumekuwa chachu ya kuanza kwa awamu ya pili ambayo itajengwa kuanzia Gerezani mpaka Mbagala ambapo mpaka kufikia awamu ya sita kutalifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa la kisasa na salama zaidi na hivyo kuwa Jiji kuu la Biashara.
Rais Magufuli amewataka watanzania kutumia vyema miundombinu ya mabasi yaendayo haraka na pia madereva wa magari madogo kuzingatia sheria kwa kutotumia njia hizo.
Rais Magufuli ametoa shukrani kwa Benki ya Dunia kwa ushirikiano wao mkubwa katika kufanikisha mradi huu na miradi mingine nchini na kuwataka kusaidia katika kufanikisha mradi wa kujengwa kwa barabara za juu katika eneo la Ubungo na wale wote wanaohusika katika kupata mkandarasi wafanikishe haraka suala hilo ili kusaidia mabasi yaendayo haraka kupita kwa urahisi na hivyo kutimiza dhana halisi ya mabasi hayo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.