Habari za Punde

TAASISI YA MOYO YAPATA WAGENI KUTOKA VYUO VIKIKUU VYA WITWATERSRAND CHA NCHINI AFRIKA YA KUSINI NA MINESSOTA CHA NCHINI MAREKANI

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaonyesha wageni kutoka Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini sehemu ya malipo ambapo wagonjwa wanalipia huduma. Wageni hao walitembelea Taasisi hiyo hivi karibuni ili kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozifanya  pia waliahidi kuimarisha  mahusiano kati yao  hii ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa madaktari wataokwenda kusoma katika chuo hicho.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Prof. Martin Valler Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Afya wa Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini wakiangalia jinsi upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) unavyofanyika katika chumba Cath Lab kilichopo katika Taasisi hiyo.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea jinsi upasuaji wa Magonjwa ya Moyo unavyofanyika katika taasisi hiyo wakati wageni kutoka Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini  walipotembelea wodi aliyokuwa amelazwa mmoja wa wagonjwa aliyefanyiwa upasuaji. Kutoka kulia ni  Prof. Martin Valler, akifuatiwa na Afisa Muuguzi Roger Kibula, watatu kulia ni Prof. Simon Nemutandani na wa pili kushoto ni Dkt. Marion Bergman.

  Daktari bingwa  wa Magonjwa ya Moyo na Mhadhili kutoka chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi  na Tiba Muhimbili (MUHAS) Prof. Johnson Rwakatare akimuonyesha vipimo vya moyo (ECHO) Prof. Martin Valler Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Afya wa Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza wataalamu wa afya kutoka Chuo Kikuu cha Minnesota cha nchini Marekani huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa wakati  walipoitembelea  Taasisi hiyo hivi karibuni. Picha na Anna Nkinda - JKCI

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.