Habari za Punde

TETESI NAHODHA WA TOGO EMMANUEL ADEBAYOR KUTUA YANGA?

Kiungo wa zamani wa Manchester City, Real Madrid, Tottenham Hotspur, Arsenal , Crystal Palace na Monaco ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Togo, Emmanuel Adebayor anatajwa kuwa muda wowote kuanzia sasa ataweza kujiunga na klabu ya Yanga ya Tanzania kwa mkataba mnono.
Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa huenda nahodha huyo wa timu ya Togo kuwa atajiunga na timu hiyo ili waweze kutetea ubingwa na kujianda na michuano ya kimataifa ya klabu bingwa Afrika.
Adebayor anataka kujiunga na wanajangwani hao ikiwa ni siku chache baada ya timu yao ya Taifa ya Togo kutolewa katika michuano ya AFCON.
Adebayor kama atajiunga na klabu hiyo ya Yanga atakuwa mchezaji wa kwanza kutoka ligi ya mabingwa ulaya kuja kucheza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.