Habari za Punde

TFF YATANGAZA KUACHANA NA MKWASA NA KUMTANGAZA MAYANGA KOCHA MPYA STARS

Na Asia Mohamed, Dar
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi leo ametangaza rasmi kuachana na kocha Boniface Mkwasa na kum
tangaza Salum Mayanga kuwa kocha mpya wa muda wa timu ya taifa, Taifa Stars.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, leo Malinzi amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kumaliza Mkataba wake leo.

Aidha alisema kuwa Kocha mpya Mayanga baada ya kutangazwa atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo zitaanza mapema mwaka huu.

Kikosi kitakachokuwa chini ya Mayanga kitakuwa ni wachezaji wa ndani kwa ajili ya mechi za kufuzu CHAN.

Malinzi alimshukuru Kocha Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 akimrithi Mholanzi, Mart Nooij na kumtakia mafanikio katika mipango yake mingine katika kuendeleza soka la Bongo.

Katika kipindi chake cha kuwa Taifa Stars, Mkwasa ameiongoza timu katika mechi 13, ikishinda mbili, kufungwa sita na sare tano.


Kikosi cha Taifa Stars kikiwa chini ya Mkwasa kimeshinda mechi mbili tu kati ya 13, ikifungwa sita na sare tano

REKODI YA MKWASA TAIFA STARS
Tanzania 1-1 Uganda (Kufuzu CHAN, Kampala)
Tanzania 1-2 Libya (Kirafiki Uturuki)
Tanzania 0-0 Nigeria (Kufuzu AFCON Dar)
Tanzania 2-0 Malawi (Kufuzu Kombe la Dunia Dar)
Tanzania 0-1 Malawi (Kufuzu Kombe la Dunia Blantyre)
Tanzania 0-2 Afrika Kusini U23 (Kirafiki Johannesburg)
Tanzania 2-2 Afrika Kusini U23 (Kufuzu Kombe la Dunia Dar)
Tanzania 2-2 Afrika Kusini U23 (Kufuzu Kombe la Dunia Dar)
Algeria 7-0 Tanzania (Kufuzu kombe la Dunia Blida)
Tanzania 1-0 Chad (Kufuzu AFCON D’jamena)
Tanzania 0-2 Misri (Kufuzu AFCON Taifa)
Tanzania 1-1 Kenya (Kirafiki Nairobi)
Tanzania 0-3 Zimbabwe (Kirafiki Harare)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.