Habari za Punde

TMAA YAJIZATITI KUKUSANYA MAPATO SEKTA YA MADINI

 Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Habari toka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Yisambi Shiwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio ya wakala huo  katika kipindi cha Julai-Desemba 2016 ikiwemo kufanikiwa kukusanya Bilioni 79.26 zilizolipwa Serikalini na Kampuni za Madini kama kodi ya mapato.kushoto ni Meneja Utafiti na Mipango wa Wakala huo BW Julius Moshi na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji na Biashara ya Madini Migodi Mikubwa,ya Kati na Midogo Mhandisi Baraka Manyama.
 Meneja Utafiti na Mipango wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bw. Julius Moshi akitoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na wakala huo katika kuhakikisha kuwa Serikali inakusanya mapato yote yanayotokana na Madini.
 .Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji na Biashara ya madini migodi mikubwa,ya kati na midogo Mhandisi Baraka Manyama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kupatikana kwa malipo ya mrabaha kutokana na shughuli za uchenjuaji wa marudio kwa kutumia teknolojia ya vat leaching.kulia ni Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza na kushoto ni Meneja Utafiti na Mipango Bw. Julius Moshi.    
 Kaimu Mkurugenzi wa ukaguzi wa hesabu za Kodi na fedha za Migodi Bw. Venance Bahati akieleza kwa waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya wakala huo kukagua migodi yote na kuhakikisha kuwa Kodi zote zinalipwa Serikalini kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya madini. kulia ni Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza na kushoto ni Meneja Utafiti na Mipango Bw. Julius Moshi. na Frank Mvungi-Maelezo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.