Habari za Punde

UHABA WA FEDHA WAKWAMISHA MAANDALIZI YA MBEGU BORA: KAMATI YA BUNGE MALIASILI

Na Debora Sanja, Bunge.
WAKALA wa Mbegu za Miti Tanzania (TSSA) unakabiliwa na uhaba wa fedha hali inayokwamisha uaandaji wa mbegu bora.
Taarifa hiyo ilitolewa Mjini Morogoro jana wakati Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea Ofisi za Wakala huo.
Akiwasilisha mada katika mkutano wa wafanyakazi wa Wakala huo na wajumbe wa Kamati ya Bunge, Mkurugenzi wa TSSA, Edger Masunga alisema kwa sasa fedha inayoapatika kwa ajili ya kuandaa mbegu bora za miti ni kidogo.
Alisema kwa sasa Wakala huo unakusanya mbegu Tani 12 badala ya tani 40 kwa mwaka na kwamba mbegu hizo wamekuwa wakiziuza katika nchi  na taasisi mbalimbali nchini.
“Changamoto nyingine tunayokabiliana nayo ni uchomaji wa misitu na miti ya asili ambapo zipo baadhi ya mbegu ambazo zipo hatarini kutoweka,” alisema.
Aidha, alisema Wakala huo unao mipango ya muda mrefu na muda mfupi ikiwemo ufunguzi wa mashamba makubwa ya mbegu za miti.
Akizungumzia majukumu ya Wakala huo, Mkurugenzi huyo alisema ni kuzalisha na kusambaza vyanzo bora vya mbegu na kuziuza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Atashista Nditiye alisema ziara hiyo ya Kamati ni ya kawaida kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya majukumu na changamoto za Wakala huo.
“Tumefanya ziara hii hapa kwa kuwa tunajua umuhimu wa Wakala huu hapa nchini,” alisema.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.