Habari za Punde

JUMUIA YJA WAZAZI KINONDONI YAADHIMISHA MIAKA 40 YA CCM KWA USAFI NA KUTOA VIFAA ZAHANATI YA KIBAMBA
Juuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, jana, Januari 28, 2017, imeadhimisha miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM, kwa kufanya usafi na kutoa vifaa mbalimbali kweye zahanati ya Kibamba, Ubugo jijini Dar es Saaam. Pichani, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya hiyo, Lucas Mgonja (wapili kulia), akikabidhi ufagio kwa Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Mwahawa Kiroboto. Kushoto ni Muuguzi Mfawishi wa Zahanati hiyo, Jesca Mpolanigwa.

Lucas Mgonja akikabidhi sabuni

Lucas Mgonja akikabidhi kifaa cha kupima homa

Lucas akikabidhi ndoo

Mgonja akikabidhi sabuni ya kufanyia usafi

Mganga Mfawidhi akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa vifaa na Mgonja

Mgonja akizungumza na Mwandishi wa habari wa Clouds Tv, Salum Mwinyimkuu, baada ya kukabidhi vifaa.

Mgonja (Wapili kushoto) akiongoza badhi ya viongozi wa Jumuia ya wazazi wilaya ya Kinondoni kukata miti na kufyeka nyasi kwenye Zahanati hiyo.

Badhi ya viongozi wa Jumuia ya wazazi wilaya ya Kinondoni wakishiriki kufanya usafi kwenye Zahanati hiyo

Mwanahawa na Mpolanigwa wakifanya usafi kwenye Zahanati hiyo

Baadhi ya viongozi wa Jumuia ya wazazi Kinondoni wakifanya usafi kwenye Zahanati hiyo

Mgonja akizungumza kabla ya yeye na ujumbe wake kuondoka kwenye Zahanati hiyo

Baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM kutoka Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinodoni wakimsikiliza Mgonja kwenye Zahanati hiyo kabla ya kuondoka.

Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akimpongeza Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi Jimbo la Ubungo, Justine Sangu, baada ya kufanya usafi na kutoa vifaa kwenye zahanati hiyo.

Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akimpongeza Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi Wilaya ya Kinondoni, Lucas Mgonja, baada ya kufanya usafi na kutoa vifaa kwenye zahanati hiyo. Picha zote na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.