Habari za Punde

WANAHABARI WAJUMUIKA KUAGA MWILI WA MWENZAO MAREHEMU AMINA JIJINI DAR LEO, KUZIKWA YANGA KESHO

Waumini wa dini ya Kiislamu wakiuswalia mwili wa marehemu Amina kabla ya kusafirishwa kuelekea Jijini Tanga.
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Amina kupakia katika gari kuanza safari kuelekea jijini Tanga.
WATU mbalimbali leo walikusanyika nyumbani kwa marehemu Amina Athuman Ukonga Banana, Dar es Salaam kutoa heshima za mwisho kabla ya mwili wake kusafirishwa kuelekea jijini Tanga kwa maziko yanayotarajia kufanyika kesho.
Akizungumza kwa niaba ya wandishi wa habari za michezo, Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa habari za Michezo TASWA, Juma Pinto alisema tasnia imeondokewa na mwandishi mchapakazi na mwadilifu.

“Kwa niaba ya wandishi wa habari za michezo tumepokea kwa masikitiko msiba wa Amina, kwani alikuwa mchapakazi na alipenda kushirikiana na wenzake,” alisema Pinto.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Uhuru Publications, Angela Akilimali alisema wamepoteza mfanyakazi hodari na pengo lake halitazibika.

“Amina alipatwa na umauti wakati akitimiza wajibu wake visiwani Zanzibar hiyo inadhihirisha wazi alikuwa mfanyakazi anayependa kutimiza wajibu wake bila kujali hali yake,” alisema Angela.

Amina alikuwa visiwani Zanzibar kikazi, kuripoti michuano ya Kombe la Mapinduzi na Mwenyezi Mungu akamuongoza kuifanya kazi yake vizuri mwanzo hadi mwisho.

Amina alipatwa na umauti usiku wa kuamkia Jumapili akiwa amelazwa Hospitali ya Mnazi Mmoja na alijifungua mtoto wa kiume ambaye kwa bahati mbaya alikwishafariki dunia.
Amina ameacha mtoto mmoja wa kike. Mungu ampumzishe kwa amani Amina Athumani. ameen

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.