Habari za Punde

WANYAMA WAZURULAO MITAANI HOVYO WAZIDI KUWA KERO KWA WAKAZI WA MBEZI JUU

Madereva wa Magari na Pikipiki wakipishana na Ng'ombe barabarani jambo ambalo ni hatari, kama walivyonaswa katika barabara ya Goba. Pamoja na Serikali kutoa matangazo kuhusu wafugaji kudhibiti wanyama wao na kutowaachia hovyo mitaani, na kwamba iwapoa wanyama watakamatwa wakizurula mitaani watachukuliwa na kupigwa mnada ama mhusika kulipa faini,lakini bado maeneo ya Mbezi juu na hasa barabara ya Goba wanyama wamekuwa wakizurula hovyo na bila wahusika kuchukua hatua.

Baadhi ya wanyama wanaoonekana wakizurula hovyo na wengine hadi usiku wa manane ni Nguruwe, Mbuzi na Ng'ombe huku wenyewe wakiwa hawajulikani kwa haraka.
Ng'ombe akijinafasi katika barabara ya Goba kwa raha zake...

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.