Habari za Punde

WATU WATATU WANUSURIKA KUUWAWA KUFUATIA TUKIO LA UJAMBAZI MKOANI KIGOMA


.

Na Rhoda Ezekiel Kigoma
WATU watatu wamenusurika kufa Mkoani Kigoma katika tukio la Unyang'anyi wa kutumia silaha lililotokea katika eneo la Zuru Manispaa ya kigoma ujijj ambapo Majambazi sita wasio julikana wakiwa na silaha aina ya SMG/SAR 01 walivamia Duka la Mpesa la Mfanya biashara ,Hussen Issa na Kuiba Kiasi cha shilingi 250,000 pamoja na simu tatu .

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa Wa Kigoma, alisema mnamo tarehe 3 Januari mwaka huu majira ya saa 20:30 usiku Huko zuru Gungu Watu sita wasio faamika waliingia dukani kwa mfanya biashara huyo kama wateja huku wakiwa wameficha siraha zao kwenye makoti baada ya Wizi huo kufanyika waliwapiga Risasi watu wa tatu katika vurugu za kufanya Wizi huo.

Mtui aliwataja walio jeruhiwa na Risasi hizo ni Hamad Kharid (36) alipigwa ubavuni ,Hussen Ndoroma (42) amejeruhiwa maeneo ya makalio na Sifa Salimu (65) amejeruhiwa na risasi miguuni ambapo risasi hiyo ilimkuta Nyumbani kwake ambapo ni jirani na wafanya biashara hao.

Aidha Mtui alisema Mpaka sasa majeruhi wanaendelea na matibabu katika hospital ya Mkoa Maweni na Jeshi la polisi linawashikilia watu wawili kwa mahojiano zaidi juu ya tukio hilo na msako mkari unaendelea kuwasaka majambazi hao wanaofanya matukio hayo ya Unyang'anyi kwa kutumia siraha.

"Niwaombe Wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi dhidi ya uhalifu ilikuunga mkono jitihada za kuondoa uhalifu kwa kutoa taarifa za waalifu wanao jihusisha na vitendo vya kiuhalifu ilihatua za kisheria ziwe zinachukuliwa dhidi yao", alisema Mtui.

Kwa Upande wake Majeruhi wa tukio hilo, Hussen Ndoroma alisema jana majira ya saa moja usiku kuna watu ambao walifika dukani kwake wakiwa waneshika panga na wengine siraha ya SMG baada ya kubishana nao ndipo walipo amua kumpiga Risasi ya Mguuni iliyotokea kwenye makalio ndipo ilipoenda kumpiga Mwanamke mmoja aliekuwa Nyumba kwake.

Alisema majambazi hao walifanikiwa kuchukua kisasi cha shilingi 250,000 pamoja na simu tatu na kuingia duka la Mwenzake Ahmadi Kharid aliekuwa akiomba msaada mwenzake asaidiwe ndipo walipo mpiga risasi eneo la ubavu wa Kushoto.

Hata hivyo Sifa Salim ambae pia nae ni miongoni mwa majeruhi hao alisema Yeye akiwa Nyumbani kwake maeneo ya zuru akiendelea na Shughuli zake za nyumbani alishtukia kitu kinakuja na kumpiga maeneo ya miguuni na kushtukia damu zikiendelea kitoka hakujua tatizo ninini.

Nae Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma Maweni Fadhiri Kibaya alikili kupokea majeruhi hao wakiwa katika hali mbaya na majeraha yao yaki vuja damu kwa Wingi ndipo walipo wachukua na kuanza kuwafanyia matibabu , mpaka sasa hili zao ni nzuri na wagonjwa wanaendelea na mayibabu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.