Habari za Punde

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA KAMATI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YA KUSHUGHULIKIA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba  (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wa Kuu wa Kitaifa. Wajumbe wa Kamati walifanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Omary Seif Abeid na Bw. Mihayo Juma N'hunga Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora  (aliyesimama) akiongea na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wa Kuu wa Kitaifa, mara baada ya kufanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Muungano Bw. Baraka Rajab Baraka.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wa Kuu wa Kitaifa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.
*********************************************
Evelyn Mkokoi na Lulu Mussa
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar (SMZ) ambao pia ni wajumbe wa kamati ya Kusimamia viongozi wakuu wa kitaifa wamekutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Masuala ya Muungano na Mazingira Mh. January Makamba, Jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo la kuzungumzia baadhi ya changamoto za Muungano na kubadilishana mawazo katika maeneo ya Muungano.

Waziri Makamba aliwapongeza wajumbe wa Kamati hiyo, na  kusema kuwa ujio wao unaonyesha dhamira nzuri ya kuwawakilisha wananchi wa Zanzibar na kuimarisha Muungano uliodumu kwa miaka hamsini na saba (53) sasa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Omary Seif Abeid ambaye pia ni Muwakilishi wa Jimbo la Konde Pemba, alisema kuwa, pande hizi mbili za Muungano hazina Budi kuwakumbuka waasisi wa Muungano huo Hayati Mzee Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuunganisha pande mbili hizi na kupatikana kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema  kuwa anaeubeza Muungano anajibeza mwenyewe.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.