Habari za Punde

WAZIRI MKUU AMJULIA HALI MAJIMAREFU KAIRUKI HOSPITALI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar es salaam akitibiwa Januari 2, 2017. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
************************************************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Steven Ngonyani (Profesa Majimarefu) aliyelazwa katika Hospitali ya Kairuki akipatiwa matibabu.

Akiwa hospitalini hapo leo (Jumatatu, Januari 2, 2017), Waziri Mkuu amesema amefurahi baada ya kumkuta Mbunge huyo anaendelea vizuri na kwamba afya yake inaridhisha.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumtakia afya njema Mhe. Ngonyani. Amesema anaamini hivi karibuni atapona na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Kwa upande wake Mbunge huyo ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, amemshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kumjulia hali.

Pia amesema anaendelea vizuri na anatarajia kwenda nchini India kwa matibabu zaidi mara taratibu zitakapokamilika.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
JUMATATU, JANUARI 2, 2017.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.